Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 6

Yusuf 12:6

يوسف

وَكَذَٰلِكَ يَجْتَبِيكَ رَبُّكَ وَيُعَلِّمُكَ مِن تَأْوِيلِ ٱلْأَحَادِيثِ وَيُتِمُّ نِعْمَتَهُۥ عَلَيْكَ وَعَلَىٰٓ ءَالِ يَعْقُوبَ كَمَآ أَتَمَّهَا عَلَىٰٓ أَبَوَيْكَ مِن قَبْلُ إِبْرَٰهِيمَ وَإِسْحَـٰقَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Maana

Na hivyo ndivyo Mola wako Mlezi atakuteua na atakufundisha katika tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya ukoo wa Yaa'qub, kama alivyowatimizia hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kadhaalika Mola wako Mlezi atakuteuwa na atakufundisha tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema zake juu yako na juu ya ukoo wa Yaa'qub, kama alivyo watimizia hapo zamani baba zako Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako Mlezi ni Mjuzi Mwenye hikima. [6]

[6] Kama ulivyo jiona katika ndoto kuwa ni bwana wa kut'iiwa, mwenye cheo na madaraka, basi Mola wako Mlezi atakuteuwa na atakukhitari, akufunze kufasiri ndoto, kwa kukupa Unabii na Utume, kama hapo zamani, kabla ya baba yako, Yaa'qub, alivyo wafanyia baba zako, Ibrahim na Is-haq. Hakika Mola wako Mlezi ni mwingi wa hikima, basi hakosei. Ni mwingi wa ujuzi, basi humteuwa katika waja wake anaye mjua kuwa anastahili kuteuliwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kama Alivyokuonesha Mola wako ndoto hii, pia Atakuteua na Atakufundisha kutafsiri ndoto ambazo watu huziona usingizini, ujue matokeo yake ya uhakika, na atazitimiza neema zake kwako na kwa kizazi cha Ya‛qûb, kama alivyozitimiza hapo nyuma kwa wazazi wako wawili, Ibrãhîm na Is’ḥãq, kwa kuwapa unabii na utume. Hakika Mola wako Anamjua yule Anayemteua miongoni mwa waja Wake, ni Mwingi wa hekima katika kuendesha mambo ya viumbe vyake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net