Yusuf 12:5
يوسفقَالَ يَـٰبُنَىَّ لَا تَقْصُصْ رُءْيَاكَ عَلَىٰٓ إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا۟ لَكَ كَيْدًا ۖ إِنَّ ٱلشَّيْطَـٰنَ لِلْإِنسَـٰنِ عَدُوٌّ مُّبِينٌ
(Baba) akasema: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wakaja kukufanyia njama. Hakika Shetani ni adui aliye dhahiri kwa mwanadamu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
(Baba) akasema: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wasije wakakufanyia vitimbi. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu. [5]
[5] Baba yake akamwambia: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako hii. Itakuja watia husda katika nyoyo zao, na Shetani atawachochea wazue njama kukupinga. Watakuja kufanyia hila na vitimbi! Hakika Shetani ni adui wazi wa binaadamu!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ya‛qûb, amani imshukie, alisema kumwambia mwanawe Yûsuf, «Ewe Mwanangu, usiwatajie ndugu zako ndoto hii, watakuhusudu, watakufanyia uadui na watafanya hila za kukuua, hakika Shetani kwa binadamu ni adui ambaye uadui wake uko waziwazi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net