Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 12 · Aya ya 11

Yusuf 12:11

يوسف

قَالُوا۟ يَـٰٓأَبَانَا مَا لَكَ لَا تَأْمَ۫نَّا عَلَىٰ يُوسُفَ وَإِنَّا لَهُۥ لَنَـٰصِحُونَ

Maana

Wakasema: Ewe baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yusuf? Na hakika sisi ni wenye kumtakia heri!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wakasema: Ewe baba yetu! Una nini hata hutuamini kwa Yusuf? Na hakika sisi ni wenye kumtakia kheri! [11]

[11] Baada ya kuwafikiana kumbaidisha Yusuf (kumpeleka mbali) walisema: Ewe baba yetu! Nini kinacho kutia shaka nasi hata unamtenga Yusuf nasi, wala huoni pana usalama anapo kuwa nasi? Sisi tunakuhakikishia kuwa sisi tunampenda, na tunamwonea huruma, na tunamtakia kheri, na tunamwongoza kwenye kheri. Hapati kwetu isipo kuwa mahaba, na nasiha safi kabisa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

wakasema ndugu zake Yûsuf, baada ya kuafikiana kumpoteza, «Ewe baba yetu, unani wewe hutufanyi sisi ni waaminifu juu ya Yûsufu pamoja na kuwa yeye ni ndugu yetu, na sisi tunamtakia wema na kumhurumia, tutamtunza na tutampa ushauri mzuri wa kidhati?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yusuf

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net