Yusuf 12:12
يوسفأَرْسِلْهُ مَعَنَا غَدًا يَرْتَعْ وَيَلْعَبْ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَـٰفِظُونَ
Muachilie kesho pamoja nasi, ale kwa furaha na acheze, na bila ya shaka sisi tutamhifadhi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mpeleke kesho pamoja nasi, ale kwa furaha na acheze; na bila ya shaka sisi tutamhifadhi. [12]
[12] Mwache ende nasi kesho machungani. Atastarehe kwa kula vyakula vizuri, atacheza na atafurahi. Na sisi kwa yakini tuna hima ya kumhifadhi kumkinga na madhara yoyote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
«Tuachie awe na sisi kesho tutakapotoka kwenda kwenye malisho ya wanyama wetu, apate kutembea, afurahike na acheze kwa kushindana na mfano wake miongoni mwa michezo inayofaa. Na sisi ni wenye kumtunza na kila unalomuogopea».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net