Hud 11:7
هودوَهُوَ ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ وَكَانَ عَرْشُهُۥ عَلَى ٱلْمَآءِ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۗ وَلَئِن قُلْتَ إِنَّكُم مَّبْعُوثُونَ مِنۢ بَعْدِ ٱلْمَوْتِ لَيَقُولَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ
Na Yeye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji, ili awajaribu ni nani kati yenu ndiye mzuri zaidi wa matendo. Na wewe ukisema, "Hakika nyinyi mtafufuliwa baada ya kufa" hakika wale waliokufuru watasema, "Haya si isipokuwa uchawi ulio wazi."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na Kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji, ili akufanyieni mtihani ajuulikane ni nani miongoni mwenu mzuri zaidi wa vitendo. Na wewe ukisema: Nyinyi hakika mtafufuliwa baada ya kufa; wale walio kufuru husema: Hayakuwa haya ila ni uchawi uliyo wazi. [7]
[7] Na Mwenyezi Mungu kaziumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake katika siku sita. Na kabla ya hapo palikuwa hapana chochote zaidi kuliko ulimwengu wa maji, na juu yake A'rshi, Kiti cha Enzi cha Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ameumba ulimwengu wote huu ili adhihirishe kwa kukujaribuni hali zenu, enyi watu, atokeze kati yenu anaye mkubali Mwenyezi Mungu kwa ut'iifu na vitendo vyema, na nani anaye yaacha hayo...Na juu ya uwezo huu wa kuumba, ukiwaambia kwa yakini: Nyinyi mtafufuliwa kutoka makaburini kwenu, na kwamba wao wameumbwa ili wafe na wafufuliwe, wao mbio mbio wanakurudi kwa mkazo kuwa haya mliyo kuja nayo hayana ukweli wowote! Wala hayo si chochote ila ni kama uchawi ulio wazi wa kuchezea akili tu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Yeye Ndiye Ambaye Aliumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake kwa Siku Sita na Arshi Yake ilikuwa iko juu ya maji kabla ya hapo, Apate kuwajaribu nyinyi, ni nani kati yenu mzuri zaidi wa utiifu na utendaji. Utendaji wenye kumtakasia Allah Mtukufu, wenye kulingana na vile Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), alivyokuwa. Na lau utasema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina wa watu wako, «Nyinyi mtafufuliwa mkiwa hai baada ya kufa kwenu.» Watafanya haraka kukanusha na watasema, «Haikuwa hii Qur’ani unayotusomea isipokuwa ni uchawi ulio wazi».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net