Hud 11:6
هودوَمَا مِن دَآبَّةٍ فِى ٱلْأَرْضِ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا ۚ كُلٌّ فِى كِتَـٰبٍ مُّبِينٍ
Na hakuna mnyama yoyote katika ardhi isipokuwa riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote hayo yako katika Kitabu chenye kubainisha.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
NA HAKUNA mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Naye anajua makao yake na mapitio yake. Yote yamo katika Kitabu chenye kubainisha. [6]
[6] Na wajue watu hawa kuwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na neema zake, na ujuzi wake, umeenea kila kitu. Basi hapana mnyama anaye furukuta katika ardhi ila Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake kesha mtengenezea riziki yake inayo wafikiana naye katika hali mbali mbali. Naye anajua anakaa wapi katika hali ya uhai wake, na pahala atapo wekwa wakati wa kufa kwake! Kila kitu katika hayo kimekwisha dhibitiwa kwake Subhanahu katika Kitabu chenye kuweka wazi hali zote ziliomo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Amechukua dhamana kuviruzuku vyote vinavyotambaa kwenye uso wa ardhi, kwa hisani Yake, na Anajua mahala pa kutulia kwake katika uhai wake na baada ya kufa kwake, na Anajua mahala ambapo vitakufa. Yote hayo yameandikwa kwenye Kitabu kilichoko kwa Allah Mtukufu chenye kueleza yote hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net