Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 5

Hud 11:5

هود

أَلَآ إِنَّهُمْ يَثْنُونَ صُدُورَهُمْ لِيَسْتَخْفُوا۟ مِنْهُ ۚ أَلَا حِينَ يَسْتَغْشُونَ ثِيَابَهُمْ يَعْلَمُ مَا يُسِرُّونَ وَمَا يُعْلِنُونَ ۚ إِنَّهُۥ عَلِيمٌۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Maana

Hebu angalia! Ati wanafunika vilivyomo vifuani mwao ili wamfiche Mwenyezi Mungu! Jueni kuwa wanapojigubika nguo zao, Yeye anajua yale wanayoyaficha na yale wanayoyaweka hadharani. Hakika Yeye ni Mwenye kujua zaidi yaliyomo vifuani.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hebu angalia! Ati wanafunika vilivyomo vifuani mwao ili wamfiche Mwenyezi Mungu! Jueni kuwa wanapo jigubika nguo zao Yeye anajua wanayo yaficha na wanayo yatangaza. Hakika Yeye ni Mjuzi wa yaliyomo vifuani. [5]

[5] Watu wanafunika vifua vyao kujaribu kuficha yanayo wapitia humo. Wanajitahidi kuficha, wakidai makusudio ya hayo ni kumficha Mwenyezi Mungu asijue hisiya za nyoyo zao! Hebu nawajue watu hawa kuwa hata wanapo kwenda kulala vitandani mwao, na wakavaa nguo zao za kulalia, na wakajisitiri na kiza cha usiku na usingizi, na kujifunika vifua, basi hapana shaka yoyote kuwa Mwenyezi Mungu anawajua, wakificha au wakitangaza. Kwani Yeye anayajua yaliyomo vifuani, na yanayo funikwa ndani yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika washirikina hawa wanaficha ukafiri katika nyoyo zao wakidhani kwamba yale ambayo nafsi zao zinayadhamiria yanafichika kwa Allah Mtukufu. Kwani hawajui wanapoifunika miili yao kwa nguo zao kwamba hayafichiki kwa Allah Mtukufu mambo yao ya siri na ya wazi? Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila ambacho vifua vyao vinakifunika miongoni mwa nia, madhamirio na siri.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net