Hud 11:4
هودإِلَى ٱللَّهِ مَرْجِعُكُمْ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ
Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu tu. Naye ni Muweza wa kila kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu tu. Naye ni Muweza wa kila kitu. [4]
[4] Marejeo yenu ni kwa Mwenyezi Mungu peke yake hapa duniani na Siku ya Kiyama, atakapo kufufueni kutoka makaburini mwenu, ili akulipeni kwa vitendo vyenu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu. Kwani Yeye ndiye aliye kamilika uwezo wake, na hashindwi na kitu chochote.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni kwa Allah Mtukufu marejeo yenu baada ya kufa kwenu nyote, basi jitahadharini na mateso Yake. Na Yeye, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake, ni Muweza wa kuwafufua nyinyi, kuwakusanya na kuwalipa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net