Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 3

Hud 11:3

هود

وَأَنِ ٱسْتَغْفِرُوا۟ رَبَّكُمْ ثُمَّ تُوبُوٓا۟ إِلَيْهِ يُمَتِّعْكُم مَّتَـٰعًا حَسَنًا إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى وَيُؤْتِ كُلَّ ذِى فَضْلٍ فَضْلَهُۥ ۖ وَإِن تَوَلَّوْا۟ فَإِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ كَبِيرٍ

Maana

Na ili mumwombe msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atawastarehesha starehe nzuri mpaka muda maalumu. Na atampa kila mwenye fadhila, fadhila yake. Na wakikengeuka, basi mimi hakika ninawahofia adhabu ya hiyo Siku Kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na ili mumwombe msamaha Mola wenu Mlezi, kisha mtubie kwake. Atakustarehesheni starehe nzuri mpaka muda maalumu. Na atampa kila mwenye fadhila, fadhila yake. Na ikiwa mtakengeuka basi mimi nakukhofieni adhabu ya hiyo Siku Kubwa. [3]

[3] Mnyenyekeeni Mwenyezi Mungu na huku mnamwomba akusameheni dhambi zenu. Kisha rejeeni kwake kwa kumuabudu kwa ikhlasi na vitendo vyema, ili apate kukustarehesheni starehe nzuri duniani mpaka utakapo kufikieni muda wenu uliyo kadiriwa, na apewe Akhera kila mwenye vitendo vyema malipo ya kazi yake na fadhila yake. Na pindi mkiyaacha haya ninayo kuitieni kwayo itakuwa mtajiletea adhabu. Na mimi nakukhofieni adhabu hii katika Siku Kubwa watakapo fufuliwa watu wote, na kutokea vitisho vikubwa kabisa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na muombeni Awasamehe dhambi zenu kisha mrudi Kwake hali ya kujuta, Atawapa raha katika ulimwengu wenu kwa kuwastarehesha vizuri kwa maisha mazuri humo mpaka ufikie kikomo muda wenu wa kuishi na Ampe kila mwenye wema wa elimu na matendo malipo makamilifu ya wema wake yasiyo na upungufu. Na mkiyapa mgongo yale ninayowaitia kwayo, basi nawachelea nyinyi kufikiwa na adhabu ya Siku ngumu, nayo ni Siku ya Kiyama. Hili ni onyo kali kwa aliyezipa mgongo amri za Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na akawakanusha Mitume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net