Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 2

Hud 11:2

هود

أَلَّا تَعْبُدُوٓا۟ إِلَّا ٱللَّهَ ۚ إِنَّنِى لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ وَبَشِيرٌ

Maana

Ili msimuabudu isipokuwa Mwenyezi Mungu. Hakika mimi kwenu ni mwonyaji na mbashiri nitokaye kwake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ili msimuabudu isipo kuwa Allah, Mwenyezi Mungu. Hakika mimi kwenu ni mwonyaji na mbashiri nitokae kwake. [2]

[2] Ewe Nabii! Waongoze watu kwa hii Qur'ani, na uwaambie: Msimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu tu. Na hakika mimi nimetumwa kutoka kwake ili nikuonyeni msikufuru ikakupateni adhabu yake, na nikupeni bishara njema kuwa mkiamini na mkat'ii, basi mtapata malipo yake..

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kuteremsha Qur’ani na kuzifafanua hukumu zake na kuzipambanua na kuipanga vizuri, ili mpate kumuabudu Allah Mtukufu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Mimi kwenu nyinyi, enyi watu, ni muonyaji kutoka kwa Allah Mtukufu mwenye kuwaonya mateso Yake na ni mwenye kuwabashiria habari njema ya malipo Yake mema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net