Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 8

Hud 11:8

هود

وَلَئِنْ أَخَّرْنَا عَنْهُمُ ٱلْعَذَابَ إِلَىٰٓ أُمَّةٍ مَّعْدُودَةٍ لَّيَقُولُنَّ مَا يَحْبِسُهُۥٓ ۗ أَلَا يَوْمَ يَأْتِيهِمْ لَيْسَ مَصْرُوفًا عَنْهُمْ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

Maana

Na hata tukiwacheleweshea adhabu mpaka muda uliokwishahisabiwa, wao hakika watasema, "Ni nini kinachoizuia?" Jueni! Siku itakapowajia, basi haitaondolewa kwao. Na yatawazingira yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukiwacheleweshea adhabu mpaka muda ulio kwisha hisabiwa wao husema: Nini kinacho izuia hiyo adhabu? Jueni! Siku itakapo wajia basi haitoondolewa hiyo kwao. Na yatawazunguka yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha. [8]

[8] Ilivyo kuwa hikima yetu ni kuakhirisha adhabu ya ukafiri wao hapa duniani mpaka wakati tuliyo uweka, nao ni Siku ya Kiyama, wao husema kwa kejeli: Nini kinacho mzuia hivi sasa? Na ailete hiyo adhabu ikiwa anasema kweli katika hiyo ahadi yake! Basi nawajue hao kwamba adhabu itakuja tu bila ya muhali. Na itapo wajia hawatapata kuokoka, na itawazunguka kwa sababu ya kejeli zao na kutaka kuvunja hishima.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau tutawacheleweshea adhabu, hawa washirikina, mpaka muda maalumu, wakaona imekawia, watasema kwa njia ya shere na kukanusha, «Ni kitu gani kinachozuia adhabu hii isitokee ikiwa ni kweli?» Jueni mtanabahi, siku itakapowajia adhabu hiyo hakuna atakayeweza kuwaondolea, wala yoyote mwenye kuizuia, na itawazunguka wao, kutoka kila upande, adhabu waliokuwa wakiifanyia shere kabla haijawajia.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net