Hud 11:9
هودوَلَئِنْ أَذَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ مِنَّا رَحْمَةً ثُمَّ نَزَعْنَـٰهَا مِنْهُ إِنَّهُۥ لَيَـُٔوسٌ كَفُورٌ
Na tukimwonjesha mtu rehema kutoka kwetu, kisha tukaiondoa kwake, yeye hakika ni mwenye kukata tamaa, mwingi wa kukufuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tukimwonjesha mtu rehema inayo toka kwetu, kisha tukamwondolea, hukata tamaa akakufuru. [9]
[9] Na katika tabia za binaadamu ni kujizamisha mwenyewe katika hali aliyo nayo. Basi tukimpa baadhi ya neema na rehema, kama vile afya nzuri, na ukunjufu wa riziki, kisha baadae tukamwondolea neema hizo, kwa mujibu wa mipango yetu, yeye hupita mipaka katika kukata tamaa kuwa neema hiyo haitorudi tena; na akapita mipaka katika kuzikufuru neema nyengine ambazo bado angali anastarehe nazo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau tutampa mwanadamu neema ya afya na amani na zisokuwa hizo kisha tukamuondolea, hakika yeye atakuwa ni mwenye kukata tamaa sana na rehema za Allah Mtukufu, ni mkanushaji sana wa neema ambazo Allah Mtukufu Amemneemesha nazo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net