Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 11 · Aya ya 10

Hud 11:10

هود

وَلَئِنْ أَذَقْنَـٰهُ نَعْمَآءَ بَعْدَ ضَرَّآءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ ذَهَبَ ٱلسَّيِّـَٔاتُ عَنِّىٓ ۚ إِنَّهُۥ لَفَرِحٌ فَخُورٌ

Maana

Na tukimwonjesha neema baada ya madhara yaliyomgusa, hakika yeye husema, "Mabaya yamekwishaniondokea." Hakika yeye ni mwenye kufurahi, mwenye kujifahiri mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tukimwonjesha neema baada ya madhara yaliyo mpata husema: Taabu zimekwisha niondokea. Hakika yeye hujitapa na kutafakhari. [10]

[10] Na tukimpa neema baada ya shida aliyo kuwa nayo yeye husema: Shida zangu zote zimekwisha niondokea, wala hazitarudi tena! Na hayo humpelekea upeo wa kufurahikia starehe za dunia, na kujifakhirisha bila ya kiasi. Moyo wake huwa umeshughulika, usimshukuru Mola wake Mlezi! Hii ndiyo hali ya binaadamu wengi, wanababaika baina ya kukata tamaa na kujitapa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau tutamnyoshea mwanadamu dunia yake na tukamkunjulia riziki yake baada ya dhiki za maisha, atasema hapo, «Nimeondokewa na dhiki na shida.» Hakika yeye ni mwenye kujigamba kwa hizo neema, ni mwenye kuendelea sana katika kujifahiri na kujitukuza kwa watu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Hud

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net