Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 72

Yunus 10:72

يونس

فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَمَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ ٱلْمُسْلِمِينَ

Maana

Na mkigeuka, basi mimi sikuwaomba ujira wowote. Ujira wangu hauko isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa kwamba niwe miongoni mwa Waislamu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini mkigeuka, basi mimi sikukuombeni ujira. Ujira wangu hauko ila kwa Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu. [72]

[72] Na ikiwa mtabaki kukataa wito wangu, basi hayo hayatanidhuru mimi kitu. Kwani mimi sikufanya hivyo kwa kutaraji kupokea ujira kwenu ambao naogopa nitaukosa, kwa sababu ya kukataa kwenu! Ujira wangu mimi nautaka kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Na Yeye ameniamrisha niwe Muislamu, nimsalimishie Yeye mambo yangu yote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mkiupuuza mwito wangu, basi sikuwaomba malipo, kwa kuwa thawabu zangu ziko kwa Allah Mtukufu na malipo yangu yako juu Yake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Peke Yake hakuna mwenye ushirika na Yeye, na nimeamrishwa niwe miongoni mwa wenye kufuata hukumu Yake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net