Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 71

Yunus 10:71

يونس

وَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ نُوحٍ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦ يَـٰقَوْمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكُم مَّقَامِى وَتَذْكِيرِى بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ فَعَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلْتُ فَأَجْمِعُوٓا۟ أَمْرَكُمْ وَشُرَكَآءَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُنْ أَمْرُكُمْ عَلَيْكُمْ غُمَّةً ثُمَّ ٱقْضُوٓا۟ إِلَىَّ وَلَا تُنظِرُونِ

Maana

Na wasomee habari za Nuhu alipowaambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Ikiwa ni kukubwa kwenu kukaa kwangu nanyi na kuwakumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, nyinyi likusanyeni jambo lenu pamoja na washirika wenu, kisha jambo lenu hilo lisiwe la kufichikana kwenu, kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu!Ikiwa kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu.Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula. [71]

[71] Yanayo kupata kutoka kwa watu wako, yaliwapata Manabii walio kutangulia. Basi wasomee hawa watu, Ewe Mtume, aliyo kuteremshia Mola wako Mlezi katika Qur'ani kisa cha Nuhu, Mtume wa Mwenyezi Mungu. Alipo iona chuki na uadui wa watu wake kwa ujumbe wake, aliwaambia: Enyi watu wangu! Ikiwa kuwa pamoja nanyi kwa ajili ya kufikisha ujumbe kumekuwa ni shida juu yenu, basi mimi ni mwenye kuendelea na wito wangu, na ni mwenye kushikilia hapo hapo, na ni mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu katika hili jambo langu. Basi nyinyi na washirika wenu jifungeni madhubuti katika shauri yenu, wala msiufiche uadui wenu kwangu kabisa, wala msinipe muhula wowote kwa maovu mnayo nipangia kunitendea, kama kweli mnaweza kuniletea madhara. Kwani Mola wangu Mlezi ananilinda.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wasimulie, ewe Mtume, makafiri wa Makkah habari ya Nûh, amani imshukie, pamoja na watu wake alipowaambia, «Ikiwa imekuwa ni uzito kwenu kukaa kwangu na nyinyi kuwakumbusha hoja za Allah Mtukufu na dalili Zake, basi ni kwa Allah Mtukufu ndio mategemeo yangu, na matumaini yangu yako Kwake Yeye. Basi tayarisheni mambo yenu na waiteni washirika wenu, kisha msiyafanye mambo yenu yafichike bali yawe waziwazi yenye kuonekana, kisha amueni juu yangu mateso na mabaya mnayoyaweza wala msinipe muhula wa saa moja ya mchana».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net