Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 70

Yunus 10:70

يونس

مَتَـٰعٌ فِى ٱلدُّنْيَا ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ ٱلْعَذَابَ ٱلشَّدِيدَ بِمَا كَانُوا۟ يَكْفُرُونَ

Maana

Hiyo ni starehe ya duniani tu, kisha marejeo yao ni kwetu. Kisha tutawaonjesha adhabu kali kwa sababu ya yale waliyokuwa wakikufuru.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hiyo ni starehe ya katika dunia tu, kisha marejeo yao ni kwetu. Tena tutawaonjesha adhabu kali kwa sababu ya kukufuru kwao. [70]

[70] Wao wana starehe hapa duniani ya kudanganyika nayo. Nayo ni chache, ikiwa itachukua muda mrefu au mfupi, ukilinganisha na hayo yanayo wangojea! Kisha marejeo yao ni kwetu, Sisi. Tutawahisabia na tutawaonjesha adhabu ya kutia uchungu kwa sababu ya ukafiri wao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wao wanastarehe ulimwenguni, kwa ukafiri wao na urongo wao, starehe fupi. Kisha ukomapo muda wao wa kuishi, kuja kwetu ndio mwisho wao. Kisha tutawaonjesha adhabu ya Jahanamu kwa kumkufuru kwao Allah Mtukufu, kukanusha kwao Mitume wa Allah Mtukufu na kupinga kwao aya Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net