Yunus 10:69
يونسقُلْ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ
Sema, "Hakika wale wanaomzulia uongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Hao wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa. [69]
[69] Ewe Mtume! Waambie: Hao wanao mtungia Mwenyezi Mungu uwongo, na wanadai kuwa ana mwana, hawatafanikiwa milele.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, «Hakika wale ambao wanamzulia Allah Mtukufu urongo, kuwa Amejifanyia mwana na mshirika, hawatapata matakwa yao ulimwenguni wala Akhera».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net