Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 68

Yunus 10:68

يونس

قَالُوا۟ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَـٰنَهُۥ ۖ هُوَ ٱلْغَنِىُّ ۖ لَهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ إِنْ عِندَكُم مِّن سُلْطَـٰنٍۭ بِهَـٰذَآ ۚ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ

Maana

Walisema, "Mwenyezi Mungu alijifanyia mwana." Ametakasika! Yeye ndiye asiyehitajia kitu. Ni vyake vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Nyinyi hamna uthibitisho wowote wa haya! Je, mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyoyajua?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wamesema: Mwenyezi Mungu ana mwana. Subhanahu, Aliye takasika! Yeye ni Mkwasi, Mwenye Kujitosheleza. Vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi ni vyake peke yake. Nyinyi hamna uthibitisho wowote wa haya! Mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua? [68]

[68] Na ikiwa wanao abudu masanamu wamefanya ushirikina wa kuabudu mawe, na hawakumtakasa Mwenyezi Mungu kwa haki ya kumtakasa, na wakasema kuwa Allah, Mwenyezi Mungu, ana mwana, basi Mwenyezi Mungu ametakasika na hayo. Yeye hana haja ya kuwa na mwana; kwani kuwa na mwana kunaonyesha wazi kutaka kubakia ukoo wako baada ya kufa kwako. Na Mwenyezi Mungu hafi. Yeye ni Mwenye kubakia milele. Na vyote viliomo katika mbingu na viliomo katika ardhi ni vyake, vimeumbwa na vinaendeshwa na Yeye. Na nyinyi wazushi, hamna hoja yoyote wala dalili ya hayo mnayo zua! Basi msikhitalifiane juu ya Mwenyezi Mungu kwa mambo yasiyo na msingi wa hakika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Washirikina walisema, «Allah Mtukufu amejifanyia mwana» kama vile wanavyosema: ‘Malaika ni watoto wa kike wa Allah Mtukufu’, au ‘Al- Masîh ni mwana wa Allah Mtukufu’. Allah Mtukufu Ametakasika na hayo yote Yeye Ndiye Mkwasi Asiyemuhitajia kila asiyekuwa Yeye. Ni Vyake Yeye vyote vilivyoko kwenye mbingu na ardhi. Vipi basi Atakuwa na mwana miongoni mwa Aliyewaumba na hali ni kwamba kila kitu kinamilikiwa na Yeye? Na nyinyi hamuna dalili yoyote juu ya urongo mnaouzua. Je, mnasema kuhusu Allah Mtukufu maneno msiyoyajua ukweli wake na usawa wake?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net