Yunus 10:67
يونسهُوَ ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيْلَ لِتَسْكُنُوا۟ فِيهِ وَٱلنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ
Yeye ndiye aliyewawekea usiku ili mtulie humo, na mchana wa kuonea. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kaumu wanaosikia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Yeye ndiye aliye kujaalieni usiku mpate kutulia humo, na mchana wa kuonea. Hakika katika haya zipo Ishara kwa watu wanao sikia. [67]
[67] Hakika huyo Mwenye kumiliki viliomo katika mbingu na ardhi, ndiye aliye kuumbieni usiku mpate kupumzika na mahangaiko ya mchana. Na amekuumbieni mchana wenye kuangaza mpate kufanya kazi na mshughulikie maslaha yenu. Hakika katika kuumbwa usiku na mchana zipo dalili zilizo wazi kwa wenye kusikia na wakapima.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yeye Ndiye Ambaye Amewaekea nyinyi, enyi watu, usiku ili mtulie ndani yake na mpumzike na usumbufu wa harakati za kutafuta maisha, na Amewaekea mchana ili muone ndani yake na muende mbio kutafuta riziki yenu. Hakika katika kupishana usiku na mchana na hali ya watu katika vipindi viwili hivyo pana dalili na hoja, kwa watu wanaozisikia hoja hizi na kuzitafakari, kwamba Allah Mtukufu, Peke Yake, Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net