Yunus 10:66
يونسأَلَآ إِنَّ لِلَّهِ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ ۗ وَمَا يَتَّبِعُ ٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ شُرَكَآءَ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ
Jueni kuwa ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyo katika mbingu na katika ardhi. Na wala hawafuati hao wanaoomba badala ya Mwenyezi Mungu washirika wowote. Wao hawafuati isipokuwa dhana tu, na hawasemi isipokuwa uongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Jueni kuwa ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na ardhinii.Na wala hawawafuati hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ni washirika wake. Wao hawafuati ila dhana tu, na hawasemi ila uwongo. [66]
[66] Enyi watu! Jueni kuwa ni vya Mwenyezi Mungu peke yake vyote viliomo mbinguni na duniani, kwa kuviumba, na kuvimiliki, na kuviendesha. Na hao wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu kwa hakika hawawafuati hao miungu ya ushirikina. Hao si chochote ila wanafuata mawazo tu, wanadhani kuwa uwezo umo katika vitu ambavyo havijifai wenyewe, la kwa manufaa wala madhara.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Jueni mtanabahi kwamba ni wa Allah Mtukufu kila aliye mbinguni au ardhini miongoni mwa Malaika, binadamu, majini na wengineo. Na ni nini wanachofuata wale wanaowaomba asiyekuwa Allah Mtukufu katika hao washirika? Hawana wanachokifuata isipokuwa shaka, na wao hawana lolote isipokuwa wanasema urongo katika yale ambayo wanamnasibisha nayo Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net