Yunus 10:73
يونسفَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيْنَـٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِى ٱلْفُلْكِ وَجَعَلْنَـٰهُمْ خَلَـٰٓئِفَ وَأَغْرَقْنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا ۖ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلْمُنذَرِينَ
Lakini wakamkadhibisha. Kwa hivyo tukamwokoa, pamoja na wale waliokuwa naye, katika jahazi. Na tukawafanya wao ndio waliobakia, na tukawazamisha wale waliozikadhibisha Ishara zetu. Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walioonywa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakamkanusha. Basi tukamwokoa, pamoja na walio kuwa naye, katika jahazi. Na tukawafanya wao ndio walio bakia, na tukawazamisha walio zikanusha Ishara zetu. Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walio onywa. [73]
[73] Na juu ya juhudi hizo, na kukakamia huko aliko kakamia Nuhu kwa ajili ya kutaka kuwaongoa hao watu wake, bado walishikilia kuendelea na kumkanusha na kumfanyia uadui. Basi Mwenyezi Mungu alimwokoa yeye pamoja na wenye kumuamini, wakapanda marikebu. Na akawajaalia hao ndio walio iamirisha nchi baada ya kuteketea makafiri, walio gharikishwa na tofani. Hebu angalia, ewe Muhammad! Vipi walio puuza onyo ulivyo malizikia mwisho wao mbaya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi wakamkanusha Nûh, watu wake katika yale Aliyowaitia kwayo kutoka kwa Allah Mtukufu. Kwa hivyo tulimuokoa Yeye na waliokuwa na Yeye kwenye jahazi, na tukawafanya wao washikilie nafasi ya waliokanusha katika ardhi, na tukawazamisha wale waliokataa hoja zetu. Hivyo basi, fikiria, ewe Mtume, namna ulivyokuwa mwisho wa watu wale ambao Mtume wao Aliwaonya adhabu ya Allah Mtukufu na mateso Yake?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net