Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 74

Yunus 10:74

يونس

ثُمَّ بَعَثْنَا مِنۢ بَعْدِهِۦ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَآءُوهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ فَمَا كَانُوا۟ لِيُؤْمِنُوا۟ بِمَا كَذَّبُوا۟ بِهِۦ مِن قَبْلُ ۚ كَذَٰلِكَ نَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلْمُعْتَدِينَ

Maana

Kisha baada yake tukawatuma Mitume kwa kaumu zao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini hawakuwa wenye kuyaamini wale waliyoyakanusha kabla yake. Hivyo ndivyo tunavyoziziba nyoyo za wavukao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha baada yake tukawatuma Mitume kwa watu wao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo wazi. Lakini hawakuwa wenye kuyaamini waliyo yakanusha kabla yake. Ndio kama hivyo tunapiga muhuri juu ya nyoyo za warukao mipaka. [74]

[74] Baada ya Nuhu tuliwatuma Mitume wengine wakilingania Tawhid, Upweke wa Mwenyezi Mungu, wakibashiria kheri na wakionya, na wakiungwa mkono na miujiza yenye kuonyesha ukweli wao. Watu wao wakawakanya kama walivyo kanya kaumu ya Nuhu. Haukuwa mwendo wa wapinzani kuwa wat'iifu, kwa sababu kule kukadhbisha kwao kulikuwa ni mbele kuliko kuzingatia na kupima. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu alipiga muhuri wa upotovu juu ya nyoyo za wale ambao mtindo wao ni kuzifanyia uadui hakika na Ishara zilizo wazi!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukatuma, baada ya Nûh, Mitume kwenda kwa watu wao (Hûd, Sãlih, Ibrãhîm, Lût, Shu‛ayb na wengineo), kila Mtume Alikuja kwa watu wake kwa miujiza yenye kuonesha dalili ya utume Wake na ukweli wa yale aliyowaitia. Hawakuwa ni wenye kuyaamini wala kuyafanya yale ambayo watu wa Nûh na waliowatangulia miongoni mwa ummah waliopita. Na kama alivyopiga mhuri Allah Mtukufu juu ya nyoyo za hawa watu wasiamini, hivyo ndivyo anavyopiga mhuri juu ya nyoyo za wanaofanana na wao kati ya waliokuwa baada yao, miongoni mwa wale ambao walivuka mipaka ya Allah Mtukufu na wakaenda kinyume na yale ambayo Mitume wao waliwaitia kwayo, ya kumtii Yeye, ikiwa ni mateso kwao kwa sababu ya matendo yao ya uasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net