Yunus 10:75
يونسثُمَّ بَعَثْنَا مِنۢ بَعْدِهِم مُّوسَىٰ وَهَـٰرُونَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَإِي۟هِۦ بِـَٔايَـٰتِنَا فَٱسْتَكْبَرُوا۟ وَكَانُوا۟ قَوْمًا مُّجْرِمِينَ
Kisha baada yao tukamtuma Musa na Haruni kwa Firauni na waheshimiwa wake, kwa Ishara zetu. Wakatakabari, na wakawa kaumu wahalifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha baada yao tukamtuma Musa na Haruni kwa Firauni na waheshimiwa wake, kwa Ishara zetu. Wakajivuna, na wakawa watu wakosefu. [75]
[75] Kisha baada yao tulimtuma Musa na ndugu yake Haruni wende kwa Firauni, mfalme wa Misri na watu wake wakuu makhsusi, kuwaita wamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake. Nao waliungwa mkono na hoja zenye nguvu. Firauni na kaumu yake walitakabari wakakataa kuitikia wito wa Musa na Haruni. Kwa kukataa kwao huko wakawa wamefanya makosa makubwa na dhambi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha tukawatuma, baada ya mitume hao, Mûsã na Hãrûn, amani iwashukie, kwenda kwa Fir‛awn na viongozi wa watu wake, wakiwa na miujiza yenye kuonesha dalili ya ukweli wao, wakafanya kiburi kwa kukataa kuikubali haki na wakawa ni watu washirikina, wahalifu na wakanushaji.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net