Yunus 10:41
يونسوَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّى عَمَلِى وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ ۖ أَنتُم بَرِيٓـُٔونَ مِمَّآ أَعْمَلُ وَأَنَا۠ بَرِىٓءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ
Na wakikukadhibisha, basi sema, "Mimi nina matendo yangu, na nyinyi mna matendo yenu. Nyinyi mko mbali sana na yale ninayoyatenda, nami niko mbali sana na mnayoyatenda."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wakikukanusha wewe, sema: Mimi nina a'mali yangu, na nyinyi mna a'mali yenu. Nyinyi hamna jukumu kwa niyatendayo, wala mimi sina jukumu kwa myatendayo. [41]
[41] Na ewe Mtume! Wakishikilia kuendelea na kukukadhibisha baada ya kuwadhihirikia wazi dalili za Unabii wako, basi wewe waambie: Hakika mimi nitalipwa kwa a'mali yangu,(vitendo vyangu); na nyinyi mtalipwa kwa a'mali yenu kama itakavyo kuwa. Na mimi naendelea na Wito wangu, na nyinyi hamtahisabiwa kwa a'mali yangu, wala mimi sitahisabiwa kwa a'mali yenu. Basi nyinyi fanyeni mpendavyo. Na Mwenyezi Mungu atamlipa kila mtu kwa aliyo yachuma.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wakikukanusha, ewe Mtume, washirikina hawa waambie, «Mimi nina Dini yangu na matendo yangu, na nyinyi muna dini yenu na matendo yenu; nyinyi hamtaadhibiwa kwa matendo yangu, na mimi sitaadhibiwa kwa matendo yenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net