Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 40

Yunus 10:40

يونس

وَمِنْهُم مَّن يُؤْمِنُ بِهِۦ وَمِنْهُم مَّن لَّا يُؤْمِنُ بِهِۦ ۚ وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِٱلْمُفْسِدِينَ

Maana

Na miongoni mwao kuna anayeiamini, na miongoni mwao kuna asiyeiamini. Na Mola wako Mlezi ndiye anayewajua vyema waharibifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwao wapo wanao iamini, na miongoni mwao wapo wasio iamini. Na Mola wako Mlezi anawajua vyema mafisadi. [40]

[40] Na miongoni mwa hawa wakanushao wapo ambao watakuja iamini Qur'ani baada ya kuyafahamu yaliyomo ndani yake, na wakayaelewa maana yake. Na kipo miongoni mwao kikundi ambacho hakiamini wala hakiachi upotovu wake! Na Allah Subhanahu wa Taa'la anawajua vyema wakanushao mafisadi, na atawalipa kwa vitendo vyao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa watu wako, ewe Mtume, kuna anayeiamini Qur’ani na miongoni mwao kuna asiyeiamini mpaka afe kwenye msimamo huo na afufuliwe juu yake. Na Mola wako anawajua zaidi hao waharibifu ambao hawaiamini kwa njia ya udhalimu, ushindani na uharibifu, na Atawalipa juu ya uharibifu wao kwa adhabu iliyo kali zaidi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net