Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 39

Yunus 10:39

يونس

بَلْ كَذَّبُوا۟ بِمَا لَمْ يُحِيطُوا۟ بِعِلْمِهِۦ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُۥ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلظَّـٰلِمِينَ

Maana

Bali waliyakadhibisha yale wasiyoyaelewa elimu yake vyema kabla hayajawajia maelezo yake. Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu hao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Bali wameyakanusha wasio yaelewa ilimu yake kabla hayajawajia maelezo yake. Kadhaalika walio kabla yao walikanusha vile vile. Basi angalia jinsi ulivyo kuwa mwisho wa madhaalimu hao. [39]

[39] Bali hawa washirikina wamekimbilia kuikadhibisha Qur'ani bila ya kuzingatia, wakajua yaliomo ndani yake! Wao wenyewe hawakutazama mna nini, wala hawakusita kuitafuta tafsiri yake, na kutaka kuelewa hukumu zake kwa kuwauliza wenginewe! Na kukadhibisha namna hii bila ya ujuzi, ndivyo walivyo wakanusha makafiri wa kaumu za zamani Mitume wao na Vitabu vyao! Basi, ewe mwanaadamu! Angalia yaliishiaje mambo ya walio kadhibisha walio tangulia. Waliachiliwa mbali na wakateketezwa kwa adhabu! Na huu ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa mfano wa hao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Bali wao walifanya haraka kuikanusha Qur’ani mwanzo walipoisikia, kabla hawajazizingatia aya zake, na wakakikanusha kitu ambacho wao hawana ujuzi nacho, miongoni mwa habari ya Ufufuzi, Malipo, Pepo, Moto na vinginevyo, na bado haujawajia wao uhakika wa yale waliyoahidiwa katika Kitabu. Na kama walivyokanusha washirikina mambo Aliyowaonya nayo Allah Mtukufu, ndivyo walivyokanusha watu waliopita kabla yao. Basi tazama, ewe Mtume, ulikuwaje mwisho wa madhalimu? Baadhi yao Allah Mtukufu Aliwaangamiza kwa kuwadidimiza ardhini, wengine kwa kuwazamisha majini na wengine kwa kuwapa mateso mengineyo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net