Yunus
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
بَلْ كَذَّبُوا۟ بِمَا لَمْ يُحِيطُوا۟ بِعِلْمِهِۦ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُۥ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَٱنظُرْ كَيْفَ كَانَ عَـٰقِبَةُ ٱلظَّـٰلِمِينَ 39
{39} Kilichowafanya waikadhibishe Qur-ani ambayo inajumuisha haki ambayo hakuna haki nyingi zaidi yake ni kwamba hawakuijua vyema. Kwa maana, lau wangeliijua vyema na wakaifahamu ipasavyo kufahamiwa, basi wangeliifuata kwa kuisadikisha. Na vile vile mpaka sasa haijawajia tafsiri yake, ambayo iliwaahidi kuwa atawateremshia adhabu, na kuwatia mateso. Na ukadhibishaji huu unaotoka kwao ni aina sawa na kule kukadhibisha kwa wale waliokuwa kabla yao. Na ndiyo maana akasema, “Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Basi angalia jinsi ulivyokuwa mwisho wa madhalimu hao.” Nayo ni maangamizo ambayo hakubaki yeyote miongoni mwao. Basi na watahadhari hawa dhidi ya kuendelea na kukadhibisha kwao, wakapatwa na yale yaliyowapata umma waliokadhibisha na vizazi vilivyoangamizwa. Na katika hili kuna ushahidi juu ya kuthibitisha mambo kwanza, na kwamba mtu hafai kuharakisha kukubali kitu au kukikataa kabla ya kukijua vyema.