Yunus 10:38
يونسأَمْ يَقُولُونَ ٱفْتَرَىٰهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا۟ بِسُورَةٍ مِّثْلِهِۦ وَٱدْعُوا۟ مَنِ ٱسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
Ama ndiyo wanasema ameizua? Sema, "Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite muwawezao, kando na Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema: Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli. [38]
[38] Bali hawa washirikina wanasema: Muhammad kaizua hii Qur'ani mwenyewe! Ewe Mtume! Waambie: Ikiwa hii Qur'ani ni kazi ya mwanaadamu, basi nyinyi leteni Sura moja tu mfano wake, na muwatake muwatakao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, waje kukusaidieni; ikiwa nyinyi ni wasema kweli katika madai yenu kuwa hii Qur'ani nimeitunga mimi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Au kwani wao wanasema kwamba Muhammad ameizua hii Qur’ani yeye mwenyewe? Wao wanajua kwamba yeye ni mwanadamu kama wao. Waambie, «Basi leteni sura moja inayofanana na hii Qur’ani katika mpango wake na uongozi wake, na takeni usaidizi wa kufanya hilo kwa mnayemuweza, badala ya Allah Mtukufu, miongoni mwa majini na binadamu, iwapo nyinyi ni wakweli katika madai yenu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net