Yunus 10:37
يونسوَمَا كَانَ هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانُ أَن يُفْتَرَىٰ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ ٱلَّذِى بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ ٱلْكِتَـٰبِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
Na haikuwa Qur-ani hii ni ya kuzuliwa kutoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini ni usadikisho wa yale yaliyoitangulia, na ni maelezo ya kina ya Kitabu kisicho na shaka yoyote ndani yake, kutoka kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na haiwezekani Qur'ani hii kuwa imetungwa na haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Lakini hii inasadikisha yaliyo tangulia, na ni mfafanuo wa Kitabu kisicho na shaka ndani yake, kutokana na Mola Mlezi wa viumbe vyote. [37]
[37] Haiwezi kutokea kuwa hii Qur'ani aizue mtu yeyote, kwani katika kuwa haiwezi kuigwa, na katika uwongofu wake, na hukumu zake, hayumkini kuwa itoke kwa yeyote isipo kuwa kwa Mwenyezi Mungu tu. Nayo inasadikisha Vitabu vya mbinguni vilivyo tangulia katika mambo ya Haki yaliyo tajwa humo, na inaweka wazi yaliyo kwisha andikwa na kuthibitishwa katika mambo ya hakika na sharia. Hapana shaka kuwa Qur'ani hii ina cheo maalumu kwa Mwenyezi Mungu, nayo ni muujiza ambao hapana mtu anaye weza kuleta mfano wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Haikuwa ni yenye kumkinika kwa yoyote kuja nayo Qur’ani hii kutoka kwa asiyekuwa Allah Mtukufu, sababu ni kwamba hakuna yoyote awezae kufanya hilo miongoni mwa viumbe. Lakini Allah Mtukufu Aliiteremsha kusadikisha vitabu alivyowateremshia Manabii Wake, kwa kuwa dini ya Allah Mtukufu ni moja. Na katika hii Qur’ani kuna maelezo na ufafanuzi wa sheria ya Allah Mtukufu Aliyowaekea ummah wa Muhammad. Hapana shaka kwamba hii Qur’ani ni wahyi unaotoka kwa Mola wa viumbe wote.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net