Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 36

Yunus 10:36

يونس

وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلَّا ظَنًّا ۚ إِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغْنِى مِنَ ٱلْحَقِّ شَيْـًٔا ۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌۢ بِمَا يَفْعَلُونَ

Maana

Na wengi wao hawafuati isipokuwa dhana tu. Na hakika, dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi yote wanayoyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Na dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika Mwenyezi Mungu anajua yote wanayo yatenda. [36]

[36] Wengi wa washirikina hawafuati katika itikadi zao ila dhana potovu zisio kuwa na dalili zozote! Na kwa jumla, dhana haifidi kitu, wala haiwezi kuwa ni badala ya kuijua Haki, na khasa ikiwa dhana yenyewe ni ya kuzua tu, kama hizi dhana za washirikina. Na hakika Mwenyezi Mungu anayajua vyema wayafanyayo wakuu wa ukafiri na wafuasi wao, naye atawalipa kwa hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wengi wa washirikina hawa hawafuati, katika kuwafanya masanamu ni waungu na kuitakidi kwao kwamba hao masanamu wanawaleta karibu na Allah Mtukufu, isipokuwa urongo na dhana, nazo hazifai kitu mbele ya ukweli. Hakika Allah Mtukufu ni Mjuzi wa wanayoyafanya washirikina hawa ya ukafiri na kukanusha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net