Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 42

Yunus 10:42

يونس

وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تُسْمِعُ ٱلصُّمَّ وَلَوْ كَانُوا۟ لَا يَعْقِلُونَ

Maana

Na miongoni mwao kuna wale wanaokusikiliza. Je, wewe unaweza wasikizisha viziwi hata kama hawatumii akili?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza. Je, wewe unaweza kuwafanya viziwi wasikie ijapo kuwa hawafahamu? [42]

[42] Na katika hawa makafiri wapo wanao kusikiliza wewe, Mtume, pale unapo waita wafuate Dini ya Mwenyezi Mungu, na hali nyoyo zao zimefungwa hazikubali Wito wako. Basi wewe huwezi kuwafanya hawa viziwi wakusikie na waongoke. Na khasa ilivyo kuwa juu ya uziwi wao, hawafahamu uyasemayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na miongoni mwa makafiri kuna wanaosikia maneno yako ya kweli na usomaji wako Qur’ani, lakini wao hawaongoki. Je, kwani wewe unaweza kuwasikizisha viziwi? Vilevile, huwezi kuwaongoa hawa isipokuwa Allah Mtukufu Atake kuwaongoa, kwa kuwa wao ni viziwi, hawaisikii haki na hawaielewi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net