Yunus 10:43
يونسوَمِنْهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تَهْدِى ٱلْعُمْىَ وَلَوْ كَانُوا۟ لَا يُبْصِرُونَ
Na miongoni mwao kuna yule anayekutazama. Je, wewe unaweza kuwaongoa vipofu hata kama hawaoni?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wapo miongoni mwao wanao kutazama. Je, wewe utawaongoa vipofu ingawa hawaoni? [43]
[43] Na wengine wapo wanao kutazama na wanalifikiria jambo lako, na wanaona dalili zilizo wazi za Unabii wako. Lakini bado hawaongoki wakafuata. Mfano wa hayo ni mfano wa kipofu, nawe huwezi kuwaongoa hao vipofu. Upofu wa macho ni kama upofu wa moyo. Wote hawana uwongofu! Kipofu haioni njia kwa kuhisi, na mpotovu haongoki kwa maana.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwao kuna wanaokutazama wewe na dalili za unabii wako wa kweli, lakini wao hawaioni nuru ya Imani Aliyokupa Allah Mtukufu. Je, unaweza, ewe Mtume, kuwaumbia vipofu macho ya kuwafanya wao waongoke. Vilevile huwezi kuwaongoa wao iwapo hawana busara. Hakika yote hayo yako kwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net