Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 16

Yunus 10:16

يونس

قُل لَّوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَا تَلَوْتُهُۥ عَلَيْكُمْ وَلَآ أَدْرَىٰكُم بِهِۦ ۖ فَقَدْ لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِّن قَبْلِهِۦٓ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

Maana

Sema, “Mwenyezi Mungu angelitaka, nisingeliwasomea, wala nisingelikuwa mwenye kukijua zaidi yenu. Kwani nilikwishakaa miongoni mwenu umri mzima kabla yake! Kwani, hamtii akilini?”

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Mwenyezi Mungu angeli taka nisingeli kusomeeni, wala nisingeli kujuvyeni. Kwani nalikwisha kaa nanyi umri mzima kabla yake! Basi, je! Hamzingatii? [16]

[16] Waambie ewe Mtume! Lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka kuwa asiniteremshie Qur'ani kutoka kwake, wala mimi nisikufikishieni, asingeli teremsha, wala mimi nisingeli kusomeeni, na wala Mwenyezi Mungu asingeli kufundisheni. Lakini Yeye kateremsha, na kanituma mimi kwayo, na mimi nimekusomeeni kama alivyo niamrisha. Na mimi nilikwisha kaa nanyi wakati mrefu kabla ya kupewa Utume, na mimi sikudai Utume wakati huo, wala sikukusomeeni kitu chochote. Na nyinyi mmeshuhudia kuwa mimi ni mkweli na muaminifu. Lakini umekuja Ufunuo na nimeamrishwa niusome. Basi hebu yatieni akilini haya mambo, na myazingatie, na yakutanisheni yaliyo pita ya zamani na ya yaliopo sasa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Waambie, ewe Mtume, «Lau Allah Mtukufu angetaka nisingewasomea hii Qur’ani, wala Allah Mtukufu Hangaliwajulisha nayo. Basi jueni kuwa hiyo ni haki itokayo kwa Allah Mtukufu. Kwani nyinyi mnajua kwamba mimi nimekaa na nyinyi muda mrefu kabla Mola wangu Hajauleta wahyi wa hiyo (Qur’ani) kwangu, na kabla sijaisoma kwenu. Basi hamtumii akili zenu kwa kuzingatia na kufikiri?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net