Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 15

Yunus 10:15

يونس

وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَاتُنَا بَيِّنَـٰتٍ ۙ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَآءَنَا ٱئْتِ بِقُرْءَانٍ غَيْرِ هَـٰذَآ أَوْ بَدِّلْهُ ۚ قُلْ مَا يَكُونُ لِىٓ أَنْ أُبَدِّلَهُۥ مِن تِلْقَآئِ نَفْسِىٓ ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَىَّ ۖ إِنِّىٓ أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّى عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ

Maana

Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji kukutana na Sisi husema, “Leta Qur-ani isiyokuwa hii, au ibadilishe.” Sema, “Haiwi kwangu niibadilishe nitakavyo mimi mwenyewe. Mimi sifuati isipokuwa yale ninayofunuliwa kwa Wahyi. Hakika mimi ninahofu, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu."

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasio taraji kukutana na Sisi husema: Lete Qur'ani isiyo kuwa hii, au ibadilishe. Sema: Hainifalii mimi kuibadilisha kwa nitakavyo nafsi yangu. Mimi sifuati ila ninayo funuliwa kwa Wahyi. Hakika mimi naogopa, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu. [15]

[15] Zilipo dhihiri Aya (Ishara) za Qur'ani kutokana na Mtume wetu Muhammad juu ya washirikina, walisema makafiri wasio ikhofu adhabu ya Mwenyezi Mungu wala hawataraji thawabu zake: Tuletee kitabu kinginecho kisicho kuwa hii Qur'ani. Au badilisha yaliyomo humu, yale yasiyo tupendeza. Waambie ewe Mtume: Hayumkini wala haijuzu mimi kugeuza au kubadilisha kwa nafsi yangu. Mimi si chochote ila ni mwenye kufuata na mwenye kufikisha kile kinacho funuliwa kwangu kutokana na Mola wangu Mlezi. Mimi naogopa, nikienda kinyume na Wahyi, Ufunuo, wa Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku ambayo khatari yake ni kuu, na kitisho chake ni kikubwa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wasomewapo washirikina aya za Allah Mtukufu zilizo wazi tulizokuteremshia wewe, ewe Mtume, husema wale ambao hawaogopi Hesabu wala hawatarajii malipo wala hawaamini Siku ya kufufuliwa na kuhuishwa, «Lete qur’ani isiyokuwa hii, au tugeuze hii Qur’ani: uifanye halali kuwa haramu na haramu kuwa halali, ahadi kuwa onyo na onyo kuwa ahadi, na uondoe yaliyomo ndani yake ya kukashifu waungu wetu na kuzifanya za kipumbavu akili zetu.» Waambie, ewe Mtume, Hilo haliko kwangu. Kwani mimi nafuata, katika kila ninalowaamrisha na ninalowakataza, yale ambayo Mola wangu Ameniteremshia na kuniamrisha kwayo. Mimi naogopa kutoka kwa Allah Mtukufu, nikienda kinyume na amri Yake, adhabu ya siku iliyo kubwa, nayo ni Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net