Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 14

Yunus 10:14

يونس

ثُمَّ جَعَلْنَـٰكُمْ خَلَـٰٓئِفَ فِى ٱلْأَرْضِ مِنۢ بَعْدِهِمْ لِنَنظُرَ كَيْفَ تَعْمَلُونَ

Maana

Kisha tukawafanya nyinyi ndio wenye kushika pahala pao katika ardhi baada yao ili tuone jinsi mtakavyotenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukakufanyeni nyiye ndio wenye kushika mahala pao baada yao katika ardhi ili tuone jinsi mtakavyo tenda. [14]

[14] Enyi Umma wa Muhammad! Tumekujaalieni muwe makhalifa wa ardhi, mshike pahala pa walio kutangulieni, ili tukujaribuni tudhihirishe mtacho kikhiari, ut'iifu au uasi, baada ya mlivyo kwisha jua yaliyo wapata walio kutangulieni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukawafanya nyinyi, enyi watu, ni badala yao katika ardhi baada ya makarne ya wale walioangamizwa, ili tuangalie vipi mtafanya: mema au maovu, tupate kuwalipa kwa hayo, kulingana na matendo yenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net