Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 13

Yunus 10:13

يونس

وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا ٱلْقُرُونَ مِن قَبْلِكُمْ لَمَّا ظَلَمُوا۟ ۙ وَجَآءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَـٰتِ وَمَا كَانُوا۟ لِيُؤْمِنُوا۟ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْقَوْمَ ٱلْمُجْرِمِينَ

Maana

Na hakika tuliviangamiza vizazi vya kabla yenu walipodhulumu, na waliwajia Mitume wao kwa Ishara zilizo wazi, lakini hawakuwa wenye kuamini. Hivyo ndivyo tunavyowalipa kaumu wahalifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kwa yakini tumekwisha ziangamiza kaumu za kabla yenu walipo dhulumu, na waliwajia Mitume wao kwa Ishara zilizo wazi; lakini hawakuwa wenye kuamini. Ndio kama hivyo tunavyo walipa watu wakosefu. [13]

[13] Na Sisi tulikwisha ziangamiza kaumu zilizo kutangulieni kwa sababu ya kufuru zao walipo wajia Mitume na Ishara zilizo wazi za kusadikisha wito wao wa kuitia Imani. Na Mwenyezi Mungu akijua, kwa ajili ya kung'ang'ania kwao ukafiri na uasi, kuwa haitopatikana Imani kwao! Basi enyi makafiri wa Kikureshi! Zingatieni! Kama tulivyo waangamiza walio kuwa kabla yenu, kadhaalika tutawalipa wakosefu kwa maangamizo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika tuliwaangamiza watu waliowakanusha Mitume wa Allah Mtukufu kabla yenu, enyi mliomshirikisha Mola wenu, waliposhirikisha na wakawajia Mitume wao kutoka kwa Allah Mtukufu wakiwa na miujiza iliyo wazi na hoja zenye kubainisha ukweli wa yale aliyekuja nayo. Basi watu hawa hawakuwa ni wenye kuwaamini Mitume wao na kuwafuata, kwa hivyo walistahili maangamivu. Na mfano wa maangamivu hayo ndivyo atakavyolipwa kila mhalifu mwenye kukiuka mipaka ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net