Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 12

Yunus 10:12

يونس

وَإِذَا مَسَّ ٱلْإِنسَـٰنَ ٱلضُّرُّ دَعَانَا لِجَنۢبِهِۦٓ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَآئِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُۥ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَآ إِلَىٰ ضُرٍّ مَّسَّهُۥ ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Maana

Na mtu akiguswa na shida, hutuomba naye ameegesha ubavu, au amekaa au amesimama. Lakini tunapomwondoshea shida yake hiyo, huendelea kama kwamba hakuwahi kutuomba tumwondoshee shida iliyomgusa. Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapitilizao viwango yale waliyokuwa wakiyatenda.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mtu akiguswa na shida hutuomba naye kaegesha ubavu, au kakaa, au kasimama. Lakini tukimwondoshea shida yake huendelea kama kwamba hakupata kutuomba tumwondoshee shida iliyo mpata. Ndio namna hiyo wamepambiwa warukao mipaka yale waliyo kuwa wakiyatenda. [12]

[12] Na mtu akisibiwa na madhara katika nafsi yake au mali yake au mfano wa hayo, huhisi unyonge wake, na humwomba Mola wake Mlezi kwa hali yoyote - akiwa kajinyoosha, au kakaa kitako, au kasimama - amwondolee dhiki zake! Mwenyezi Mungu akisha mwitikia, na akamwondolea hizo shida zake, humuacha kando Mwenyezi Mungu na akaendelea na maasi yake, na akasahau fadhila za Mwenyezi Mungu juu yake, kama kwamba hakupatikana na madhara yoyote, wala hajapata kumwomba amwondolee! Na mfano wa mtindo huu Shetani ndio huwazaini Makafiri, akawapambia vitendo vyao viovu, na uzushi wao mpotovu, wakaona yote hayo ni mazuri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na impatapo binadamu shida, anatuomba tumsaidie katika kumuondolea hiyo akiwa katika hali ya kuwa amelala kwa ubavu wake au ameketi au amesimama, kulingana na hali ile alivyo wakati mashaka yalipomshukia. Na tunapomuondolea ile shida iliyompata, huendelea kuifuata ile njia yake ya mwanzo kabla hajapatwa na mashaka na huyasahau yale aliokuwa nayo ya shida na matatizo na huacha kumshukuru Mola Wake aliyemuondolea yale aliyokuwa nayo ya matatizo. Na kama alivyopambiwa binadamu huyu kuendelea katika kukanusha kwake na kuwa na ujeuri baada ya Allah Mtukufu Kumuondolea mashaka Aliyokuwa nayo, vilevile walipambiwa wale waliopita kiasi katika kumzulia Allah Mtukufu urongo na Manabii Wake yale ambayo walikuwa wakiyafanya ya kumuasi Allah Mtukufu na kumshirikisha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net