Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 11

Yunus 10:11

يونس

وَلَوْ يُعَجِّلُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ ٱلشَّرَّ ٱسْتِعْجَالَهُم بِٱلْخَيْرِ لَقُضِىَ إِلَيْهِمْ أَجَلُهُمْ ۖ فَنَذَرُ ٱلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَآءَنَا فِى طُغْيَـٰنِهِمْ يَعْمَهُونَ

Maana

Na lau kama Mwenyezi Mungu angeliwafanyia watu haraka kuwaletea maovu kama wanavyojiharakishia kuletewa heri, basi bila ya shaka wangelikwishatimiziwa muda wao. Lakini tunawaacha wale wasiotaraji kukutana nasi wakihangaika katika upotovu wao.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kama Mwenyezi Mungu angeli wafanyia watu haraka kuwaletea shari kama wanavyo jihimizia kuletewa kheri, bila ya shaka wangelisha timiziwa ajali yao. Lakini tunawaacha wale wasio tumainia kukutana nasi wakihangaika katika upotovu wao. [11]

[11] Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli waitikia watu wanapo jiapizia shari kama vile wanavyo jihimizia kuitaka kheri, angeli waangamiza akawateketeza wote. Lakini Yeye anawachukulia kwa upole basi anaakhirisha kuwateketeza, ili kungojea wadhihirishe walio nayo kwa mujibu wa anavyo wajuulia, upate kuonekana wazi uadilifu wake kwa atavyo walipa. Wanaachwa na ushahidi wa kutosha umesimama dhidi yao, nao makusudi wanakengeuka na kuelekea njia ya upotovu na udhalimu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau Allah Mtukufu angewaharakishia watu kuyakubali maombi yao ya kujitakia mabaya kama Anavyowaharakishia katika kuwakubalia maombi yao ya kujitakia mazuri wangaliangamia. Hivyo basi tunawaacha, wale ambao hawaogopi mateso yetu wala hawaamini kidhati kufufuliwa na kuhuishwa, ndani ya uasi wao na ujeuri wao hali ya kuwa wanashangaa na kuduwaa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net