Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 17

Yunus 10:17

يونس

فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِـَٔايَـٰتِهِۦٓ ۚ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلْمُجْرِمُونَ

Maana

Basi ni nani aliye dhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu na akazikadhibisha Ishara zake? Hakika hawafaulu wahalifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi ni nani aliye dhaalimu zaidi kuliko yule anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu na akazikanusha Ishara zake? Hakika hawafanikiwi wakosefu. [17]

[17] Hapana mtu aliye jidhulumu nafsi zaidi kuliko anaye kufuru na akamzulia uwongo Mwenyezi Mungu, au akazikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu alizo kuja nazo Mtume wake. Hakika hafuzu kafiri katika vitendo vyake. Naye amekhasiri khasara iliyo wazi kwa ukafiri wake na amemghadhibisha Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hapana yoyote mwenye udhalimu mkubwa zaidi kuliko yule aliyemzulia Allah Mtukufu urongo au akazikanusha aya Zake. Hakika ni kwamba hawatafuzu waliowakanusha Manabii wa Allah Mtukufu na Mitume Wake wala hawatafaulu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net