Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 10 · Aya ya 18

Yunus 10:18

يونس

وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ وَيَقُولُونَ هَـٰٓؤُلَآءِ شُفَعَـٰٓؤُنَا عِندَ ٱللَّهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّـُٔونَ ٱللَّهَ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَلَا فِى ٱلْأَرْضِ ۚ سُبْحَـٰنَهُۥ وَتَعَـٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Maana

Nao wanaabudu badala ya Mwenyezi Mungu wale wasiowadhuru wala kuwanufaisha, na wanasema, “Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu!” Sema, “Je, mnamwambia Mwenyezi Mungu yale asiyoyajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Ametakasika na ametukuka mbali na hao wanaomshirikisha nao.”

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nao, badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasio wadhuru wala kuwanufaisha,na wanasema: Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu! Sema: Je! Mnamwambia Mwenyezi Mungu asiyo yajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Subhanahu wa Taa'la! Ametakasika na ametukuka na hao wanao mshirikisha naye. [18]

[18] Na hawa washirikina wanao mzulia Mwenyezi Mungu kuwa ana washirika, wanaabudu masanamu ya upotovu. Hayawadhuru wala hayawanufaishi. Na wanasema: Masanamu haya yatatuombea kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Akhera! Ewe Mtume! Waambie: Hivyo nyinyi mnamwambia Mwenyezi Mungu kuwa ana washirika ambao hawajui, la katika mbingu wala katika ardhi? Mwenyezi Mungu ametakasika na kuwa na washirika, na yote mnayo zua kwa kuwaabudu hao washirika.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hawa wanaomshirikisha Allah Mtukufu na asiyekuwa Yeye wanaviabudu visivyowadhuru chochote wala kuwanufaisha ulimwenguni wala Akhera, na wanasema, «Sisi tunawaabudu wao ili watuombee mbele ya Allah Mtukufu.» Waambie, ewe Mtume, «Je, mnampa habari Allah Mtukufu, Aliyetukuka, jambo Asilolijua, katika mbingu au katika ardhi, kuhusu mambo ya waombezi hawa? Kwa hakika lau kungekuwa na waombezi katika hizo wa kuwaombea nyinyi mbele Yake, Angalikuwa na ujuzi zaidi kuhusu wao kuliko nyinyi. Kwani Mwenyenyezi Mungu, Aliyetukuka, ametakasika na wanachokifanya washirikina hawa cha kushirikisha kwao, katika ibada Yake, vitu visivyodhuru wala kunufaisha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Yunus

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net