Yunus 10:19
يونسوَمَا كَانَ ٱلنَّاسُ إِلَّآ أُمَّةً وَٰحِدَةً فَٱخْتَلَفُوا۟ ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِىَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Na watu hawakuwa isipokuwa Umma mmoja tu, kisha wakahitilafiana. Na lau kuwa si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, hakuna shaka hukumu ingelikwishakatwa baina yao katika yale wanayohitilafiana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala watu hawakuwa ila Umma mmoja tu. Kisha wakakhitalifiana. Na lau kuwa si neno lililo kwisha tangulia kutokana na Mola wako Mlezi, hapana shaka hukumu ingeli kwisha katwa baina yao katika hayo wanayo khitalifiana. [19]
[19] Watu kwa maumbile yao hawakuwa ila ni Umma mmoja tu. Kisha tukawapelekea Mitume wawaongoze na wawaongoe kwa mujibu wa Ufunuo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ikawa tabia ya kibinaadamu iliyo pelekea kheri na shari ndiyo sababu ya kuwa na nguvu zaidi shari katika baadhi yao. Juu yao hao matamanio na nyendo za Shetani zikatawala, na kwa hivyo wakakhitalifiana. Na lau kuwa hukumu ya Mola wako Mlezi haikutangulia ya kuwapa muhula makafiri kwa ajili yako, Ewe Nabii, na kuakhirisha maangamizo yao mpaka siku maalumu iliyo ahidiwa, Mwenyezi Mungu angeli wapelekea upesi maangamizo na adhabu, kwa sababu ya mfarakano waliyo uingia, kama zilivyo ingia kaumu zilizo kwisha pita.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Watu walikuwa kwenye dini moja, nayo ni Uislamu, kisha wakatafautiana baada ya hapo, wakakufuru baadhi yao na wengine wakasimama imara juu ya haki. Na lau si neno lililotangulia kutoka kwa Allah Mtukufu la kuwapa muhula wenye kuasi na kutowafanyia haraka kuwapatiliza kwa madhambi yao, basi wangaliamuliwa baina yao kwa kuwaangamiza watu wa ubatilifu miongoni mwao na kuwaokoa watu wa ukweli.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net