Yunus 10:20
يونسوَيَقُولُونَ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ ءَايَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ ۖ فَقُلْ إِنَّمَا ٱلْغَيْبُ لِلَّهِ فَٱنتَظِرُوٓا۟ إِنِّى مَعَكُم مِّنَ ٱلْمُنتَظِرِينَ
Na wanasema, “Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?” Sema, “Hakika mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu. Basi nyinyi ngojeni, na mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.”
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanasema: Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu. Basi nyinyi ngojeni, na mimi ni pamoja nanyi katika wanao ngojea. [20]
[20] Na hawa washirikina wanasema: Hivyo Muhammad hateremshiwi muujiza usio kuwa hii Qur'ani, wa kutuyakinisha Utume wake? Waambie Ewe Mtume! Kuteremshwa Ishara ni jambo la ghaibu, hapana alijuaye ila Mwenyezi Mungu. Kama Qur'ani haikufaini basi ngojeni hukumu ya Mwenyezi Mungu baina yangu na nyinyi katika hayo mnayo yabisha. Na mimi ni pamoja nanyi katika wanao ngojea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na makafiri hawa wakaidi wanasema, «Basi si ateremshiwe Muhammad ujuzi, dalili na miujiza inayoonekana, kutoka kwa Mola wake, ambayo kwayo tutajua kuwa yeye yuko juu ya haki katika yale anayoyasema.» Waambie, ewe Mtume, Hakuna ajuwaye ghayb (yasioonekena) isipokuwa ni Allah Mtukufu. Akitaka (kufanya wanayoyataka) Atafanya na akitaka (kutofanya) hatafanya. Basi ngojeni, enyi watu, uamuzi wa Allah Mtukufu baina yetu na nyinyi wa kuyaharakisha mateso Yake kwa wakosa kati yetu na kumnusuru mwenye haki; mimi nalingojea hilo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net