Mtu mmoja miongoni mwa watu wa Najdi alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na nywele zake zikiwa zimetimkatimka na sauti yake ikiwa juu, wala haeleweki anasema nini, mpaka alipomkaribia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akauliza kuhusu faradhi za Uislamu? Basi Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, akaanza na swala, na akamwambia kuwa Mwenyezi Mungu amemfaradhishia kuswali swala tano katika kila mchana na usiku. Akasema: Je, ninalazimika kuswali swala zingine zaidi ya hizi tano? Akasema: Hapana, labda kama utajitolea kuswali swala za sunna. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Na miongoni mwa ibada alizokuwajibishia Mwenyezi Mungu juu yako ni kufunga mwezi wa Ramadhani. Yule bwana akasema: Je, ninalazimika kufunga funga zingine zaidi ya swaumu ya Ramadhani? Akasema: Hapana, ila kama utajitolea kufunga. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtajia Zaka Yule bwana akasema: Je, ninalazimika chochote katika sadaka baada ya zaka ya faradhi? Akasema: Hapana, ila kama utajitolea. Baada ya mtu huyo kusikia faradhi hizo kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aligeuka na kuapa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa atashikamana nazo bila ya kuongeza wala kupunguza, akasema rehema na amani zimshukie baada ya kauli yake hiyo: Ikiwa bwana huyu atakuwa mkweli kwa alichoapia, basi atakuwa miongoni mwa waliofaulu.
- Upole wa sheria ya Kiislamu na urahisi wake kwa wanaoitekeleza.
- Muamala wake mzuri rehema na amani ziwe juu yake kwa mtu huyu, kwani alimpa nafasi ya kumsogelea na kumuuliza maswali.
- Kuanza na mambo muhimu zaidi kisha yanayofuata kwa umuhimu wakati wa kuwalingania watu kwa Mwenyezi Mungu.
- Uislamu ni itikadi na matendo, matendo hayawezi kufaa bila imani, wala imani haiwezi kufaa bila matendo.
- Umuhimu wa matendo haya nakuwa matendo haya ni miongoni mwa nguzo za imani.
- Swala ya Ijumaa imejumuishwa katika sala tano za faradhi; Kwa sababu ni badala ya swala ya adhuhuri siku ya Ijumaa kwa wale ambao ni wajibu kwao.
- Mtume, rehema na amani ziwe juu yake alianza mafundisho yake kwa kutilia mkazo faradhi za Uislamu, ambazo ni nguzo zake baada ya Shahada mbili. Kwa sababu muulizaji alikuwa Muislamu, na hakutaja Hija kwa sababu tukio hili lilikuwa kabla ya kufaradhishwa kwake, au kwa sababu wakati wake ulikuwa haujafika.
- Ikiwa mtu atajiwekea mipaka katika yale yaliyo wajibu kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, atafaulu, lakini hii haimaanishi kuwa si Sunna kufanya hivyo kwa hiari; Kwa sababu sala za hiari hukamilisha sala za faradhi Siku ya Kiyama.
صحيح البخاري (1/ 18) (46). صحيح مسلم (1/ 40) (11). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين. بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 346). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 857). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 242).