Alipomtuma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Muadhi Ibn Jabal -Radhi za Allah ziwe juu yake- kwenda katika miji ya Yemen kama mlinganizi wa kuwaita watu kwa Mwenyezi Mungu na kama mwalimu, alimuweka wazi kuwa atakumbana na jamii ya Wakristo; ili awe na maandalizi, kisha aanze katika kuwaita kwake na mambo muhimu zaidi kisha yanayofuatia, Atawaita kurekebisha itikadi kwanza; washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; Kwa sababu wao kwa itikadi hiyo yakuwa hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake; wataingia katika Uislamu, ikiwa watatii hilo basi awaamrishe wasimamishe swala; kwani huo ndio wajibu mkubwa baada ya tauhidi, Watakapoisimamisha awaamrishe matajiri wao kutoa zaka ya mali zao kuwapa mafukara wao, kisha akamtahadharisha na kuchukua mali bora; kwa sababu ya wajibu ni mali ya kati na kati, Kisha akamuusia aiepuke dhulma; asijekumuombewa dua mbaya aliyemdhulumu, kwani dua yake hupokelewa.
- Maana ya kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, ni kumfanya Allah kuwa wa pekee kwa ibada, na kuacha kuabudu visivyokuwa Yeye.
- Maana ya kushuhudia kuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu; Ni kumuamini yeye na yale aliyokuja nayo na kumsadikisha, nakuwa yeye ni wa mwisho katika Wajumbe wa Mwenyezi Mungu kuja kwa wanadamu.
- Nikuwa kujadiliana na msomi mwenye hoja tata si sawa na kujadiliana na mjinga; Ndio maana alimtanabahisha Muadhi kwa kumwambia: "Hakika wewe unakwenda katika jamii ya watu wa kitabu".
- Kuna umuhimu wa muislamu kuwa na uelewa katika dini yake; ili asalimike na upotovu wa wenye kumtia utata, na hii inakuwa kwa kutafuta elimu.
- Ubatili wa dini ya Mayahudi na Wakristo baada ya kutumwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, nakuwa wao si miongoni mwa watakao okoka siku ya Kiyama mpaka waingie katika dini Uislamu, na wamuamini Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
صحيح البخاري (2/ 119) (1458)، (2/ 128) (1496)، (9/ 114) (7372). صحيح مسلم (1/ 50) (19). فتح الباري لابن حجر (13/ 349). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح فوزان (ص54). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص64).