Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu alimuamrisha kupigana na washirikina mpaka washuhudie kuwa hapana muabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu peke yake asiye na mshirika, na wamshuhudilie Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake utume, na kuyafanyia kazi makusudio ya shahada hii, ikiwemo kuhifadhi swala tano usiku na mchana, na wawape zaka za faradhi wastahiki wake. Wakifanya mambo haya basi Uislamu utakinga damu zao na mali zao, haitokuwa halali kuwaua isipokuwa watakapofanya uhalifu au kosa la jinai watakalostahiki kwalo kuuawa kwa mujibu wa hukumu za Uislamu, kisha siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atasimamia hesabu yao kwani yeye ndiye ajuaye siri zao.
- Hukumu zote huenda kulingana na kile kichodhihiri, na Allah ndiye msimamizi wa siri.
- Umuhimu wa kufikisha ujumbe wa tauhidi nakuwa ndio ujumbe wa kwanza katika ufikishaji.
- Hadithi hii haimaanishi kuwalazimisha washirikina kuingia katika Uislamu, bali wamepewa uhuru wa kuchagua kati ya kuingia katika Uislamu au kutoa Jizia (Kodi); ikiwa watakataa na wakataka kuzuia ujumbe wa Uislamu, kukawa hakuna namna nyingine zaidi ya kuwapiga vita kwa mujibu wa hukumu za kiislamu.
صحيح البخاري (1/ 14) (25). صحيح مسلم (1/ 53) (22). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل السعدي (ص23). شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص125).