Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mtume wetu Muhammad - Rehema na amani za Allah ziwe juu yake-

Hadithi 12

Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم أنه قال: «وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَا يَسْمَعُ بِي أَحَدٌ مِنْ هَذِهِ الْأُمَّةِ يَهُودِيٌّ وَلَا نَصْرَانِيٌّ، ثُمَّ يَمُوتُ وَلَمْ يُؤْمِنْ بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ إِلَّا كَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- amesema: "Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuna atayemsikia katika umma huu, Myahudi au Mkristo au mwingine yeyote utakayemfikia ujumbe wa Mtume -sala na amani ziwe juu yake- kisha akafa na hakumuamini isipokuwa atakuwa miongoni mwa watu wa motoni ataishi humo milele daima.

Mafunzo
  1. Kuenea kwa ujumbe wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa ulimwengu mzima, na ulazima wa kumfuata kwake, na kufutwa kwa sheria zote kupitia sheria yake.
  2. Atakayempinga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hayatomfaa kitu madai yake ya kudai kumwamini Nabii mwingine katika Manabii -Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao wote-.
  3. Ambaye hakumsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na haukumfikia ujumbe wa Uislamu huyu atapewa udhuru, na hukumu yake huko Akhera itakuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Yanathibitika manufaa kwa Uislamu kwa mtu hata kama atasilimu muda mchache kabla ya kifo, hata kama atakuwa katika maradhi mabaya, madama tu roho haijafika kooni.
  5. Kuiona kuwa ni sahihi dini ya makafiri -wakiwemo Mayahudi na Wakristo- ni ukafiri.
  6. Amemtaja Myahudi na Mkristo katika hadithi kama tahadhari kwa wenye kuwaona kuwa wako sawa; na hii ni kwakuwa Mayahudi na Wakristo wana kitabu, na ikiwa ndio hivyo, basi kwa wengine wasiokuwa na kitabu ndio wanastahiki zaidi kuingia motoni, wote hao wanalazimika kuingia katika dini yake na kumtii yeye Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 134) (153). شرح النووي على مسلم (2/ 186). الإفصاح عن معاني الصحاح، لابن هبيرة (8/ 192). طرح التثريب في شرح التقريب، لعبد الرحيم العراقي (7/ 159).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Tukasema: Wewe ni bwana yetu, akasema: "Bwana ni Mwenyezi Mungu", Tukasema: Na mbora zaidi kuliko sisi katika fadhila, na mtoaji zaidi kuliko sisi, akasema: "Semeni kwa maneno mliyozoea, au baadhi yake, na wala asikukokoteni Shetani

عَن عَبدِ الله بنِ الشِّخِّير رضي الله عنه قَالَ: انْطَلَقْتُ في وَفدِ بَنِي عَامِرٍ إِلى رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقُلنا: أَنتَ سيّدُنَا، فقال: «السَّيدُ اللهُ»، قُلنا: وَأَفْضَلُنا فَضْلاً، وأعظَمُنا طَوْلاً، فقال: «قُولُوا بِقَولِكُم، أَو بَعضِ قولِكُم، وَلَا يَسْتَجْرِيَنَّكُم الشَّيطَانُ».
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Shikhiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilisafiri katika msafara wa Bani Aamir kwenda kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Tukasema: Wewe ni bwana yetu, akasema: "Bwana ni Mwenyezi Mungu", Tukasema: Na mbora zaidi kuliko sisi katika fadhila, na mtoaji zaidi kuliko sisi, akasema: "Semeni kwa maneno mliyozoea, au baadhi yake, na wala asikukokoteni Shetani".
Imepokelewa na Abu Daud na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Lilikuja kundi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, walipofika kwake wakasema -kwa kumsifu- kwa baadhi ya maneno ambayo aliyachukia -Rehema na amani ziwe juu yake-, Wakasema: "Wewe ni bwana yetu", Akasema kuwaambia -Rehema na amani ziwe juu yake- "Bwana ni Mwenyezi Mungu" Yeye ndiye mwenye ubwana uliokamilika juu ya viumbe wake nao ni waja wake. Na wakasema: "Wewe ndiye mbora wetu" na mwenye daraja na utukufu wa juu kuliko sisi na mwenye sifa nyingi. Na wewe "Ndiye mtoaji zaidi kuliko sisi" na mwingi wa ukarimu na utukufu na daraja ya juu. Kisha akawaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake waseme kauli yao iliyozoeleka na wasijilazimishe kutafuta maneno mengine, na kuwa shetani asiwavute katika kuchupa mipaka na kupitiliza kunakopelekea kuingia katika yale yaliyoharamishwa miongoni mwa shirki na njia zake.

Mafunzo
  1. Utukufu wa cheo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ndani ya nafsi za Masahaba wake na heshima yao kwake.
  2. Katazo la kijikalifisha katika matamshi, na kubakia katika maneno yaliyozoeleka.
  3. Kuilinda tauhidi dhidi ya yale yanayoiharibu miongoni mwa kauli na matendo.
  4. Katazo la kuchupa mipaka katika kusifu, kwani hilo ni katika njia za Shetani.
  5. Mtume rehema na amani ziwe juu yake ndiye bwana wa watoto wa Adam, na haya yaliyotajwa katika hadithi hii ni katika sehemu ya unyenyekevu, na ni katika sehemu ya kuwahofia wao wasijekuchupa mipaka katika hilo.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 184) (4806). مسند أحمد (26/ 234) (16307). الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص424). الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص472). مشكاة المصابيح، للألباني مشكاة المصابيح (3/ 1373).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nyanyua kichwa chako na sema yasikilizwe, na omba upewe, na taka utetezi utetewe

عن أنس بن مالك رضي الله عنه مرفوعاً: أخبر النبي صلى الله عليه وسلم : "أنه يأتي فيسجد لربه ويحمده [لا يبدأ بالشفاعة أولا]، ثم يقال له: "ارفع رأسك وقل يُسمع، وسَلْ تُعط، واشفع تُشفَّع".
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: Alieleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- "kwamba yeye atakuja asujudu kwa Mola wake na amtukuze [hatoanza na kuomba utetezi kwanza], kisha ataambiwa: "Nyanyua kichwa chako na sema yasikilizwe, na omba upewe, na taka utetezi utetewe".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Atakuja Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- siku ya kiyama atasujudu kwaajili ya Mwenyezi Mungu, na aombe, kisha amuidhinishe Mwenyezi Mungu katika utetezi mkubwa, na aseme Mola wake kumwambia: Omba upewe, na taka utetezi utetewe, Yaani ombi lako ni lenye kukubalika na utetezi wako ni wenye kukubalika.

Marejeo

1- القول المفيد على كتاب التوحيد، دار ابن الجوزي، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الثانية, محرم، 1424ه. 2- صحيح البخاري، المحقق: محمد زهير بن ناصر الناصر، الناشر: دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم ترقيم محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422هـ. 3- صحيح مسلم، المحقق: محمد فؤاد عبد الباقي، الناشر: دار إحياء التراث العربي – بيروت.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Nimepewa mambo matano ambavyo hakupewa mtu mwingine miongoni mwa Manabii kabla yangu

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أُعْطِيتُ خَمْسًا لَمْ يُعْطَهُنَّ أَحَدٌ قَبْلِي: نُصِرْتُ بِالرُّعْبِ مَسِيرَةَ شَهْرٍ، وَجُعِلَتْ لِي الأَرْضُ مَسْجِدًا وَطَهُورًا، فَأَيُّمَا رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي أَدْرَكَتْهُ الصَّلاَةُ فَلْيُصَلِّ، وَأُحِلَّتْ لِي المَغَانِمُ، وَلَمْ تَحِلَّ لِأَحَدٍ قَبْلِي، وَأُعْطِيتُ الشَّفَاعَةَ، وَكَانَ النَّبِيُّ يُبْعَثُ إِلَى قَوْمِهِ خَاصَّةً وَبُعِثْتُ إِلَى النَّاسِ عَامَّةً».
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Nimepewa mambo matano ambavyo hakupewa mtu mwingine miongoni mwa Manabii kabla yangu. Nimenusuriwa na hofu kwa umbali wa safari ya mwezi mmoja. Na nimefanyiwa ardhi kuwa mahali pa kuswalia na ni twahara (safi). Hivyo, yeyote katika umma wangu atakapokutwa na swala, basi na aswali (popote). Na nimehalalishiwa ngawira. Na kila Nabii alikuwa akitumwa kwa umma wake tu, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote. Na nimepewa uombezi (Siku ya Kiyama)”.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu amempa mambo matano ambayo hakupewa yeyote katika Manabiii kabla yake: La kwanza: Nimeepushwa na hofu, na hofu hiyo inatiwa katika nyoyo za maadui zangu hata kukiwa kati yangu na wao mwendo wa kutembea mwezi mzima. La pili: Tumefanyiwa Ardhi kwetu kuwa Msikiti tuswali mahala popote tutakapokuwa, na udongo wake ni twahara (safi) pale tunaposhindwa kutumia maji. La tatu: Tumehalalishiwa ngawira za vita, nazo ni zile wanazozichukua waislamu katika vita vyao na makafiri. La nne: Nimepewa utetezi mkubwa katika kuwapumzisha watu na misukosuko ya kisimamo cha siku ya Kiyama. La tano: Nimetumwa kuja kwa viumbe wote binadam wao na majini wao, kinyume na Manabii walikokuwa kabla yake, walikuwa wakitumwa kwa watu wao pekee.

Mafunzo
  1. Sheria ya mtu kuhesabu neema za Mwenyezi Mungu juu yake kwa kuzisimulia na kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizo.
  2. Fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya umma huu na kwa Nabii wao, kwa kupewa mambo haya.
  3. Uwajibu wa kuitekeleza swala kwa wakati wake kwa hali yoyote ile itakayokuwa, na mtu afanye awezacho katika sharti zake na nguzo zake na wajibu wake.
  4. Utetezi maalumu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake unaotofautiana na wa Manabii, una aina nyingi: Ya kwanza: Utetezi wake kwa viumbe ili hukumu ipite baina yao, na pia: Utetezi wake wa kuingia watu wa peponi peponi, na pia: Utetezi wake maalumu kwa ami yake Abii Twalib katika kupunguziwa adhabu ya moto si kutolewa kwenye moto; kwa sababu alikufa kafiri.
  5. Mambo ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni mengi mno ambayo hayakutajwa katika hadithi hii yakiwemo: Alipewa mkusanyo wa maneno (maneno machache yenye maana pana), na umehitimishwa utume kupitia kwake, na zimefanywa safu zetu kuwa kama safu za Malaika, na mambo mengine mengi.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 74) (335). صحيح مسلم (1/ 370) (521). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص74). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 94).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa hakuna chochote nyumbani kwake anachoweza kukila mwenye ini (uhai) ila kiasi kidogo cha ngano kilichokuwa katika ubao wangu (wa kuhifadhia chakula), nikala mpaka kikakaa muda mrefu, nilipokipima kikamalizika

عن عائشة رضي الله عنها قالت: تُوُفِّيَ رسول الله صلى الله عليه وسلم وما في بيتي من شيء يَأكُلُهُ ذُو كَبدٍ إلا شَطْرُ شَعير في رَفٍّ لي، فأكَلتُ منه حتى طال عليَّ، فَكِلْتُهُ فَفَنِيَ.
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa hakuna chochote nyumbani kwake anachoweza kukila mwenye ini (uhai) ila kiasi kidogo cha ngano kilichokuwa katika ubao wangu (wa kuhifadhia chakula), nikala mpaka kikakaa muda mrefu, nilipokipima kikamalizika
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alifariki hali yakuwa hakuna nyumbani kwake chochote isipokuwa kiasi kidogo cha ngano, na maana yake ni kiwango kidogo cha ngano, kama alivyoifasiri imamu Tirmidhiy, akaendelea kula katika chakula alichokiacha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa muda mrefu, alipokipima kikamalizika, na hii ni ishara ya kuendelea kwa baraka zake -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chakula hicho kidogo, pamoja na kutokuwepo kwa kipimo kinachoonyesha kiasi wakati wa kumtegemea Mwenyezi Mungu, kipimo wakati wa kuuziana kinahitajika kwaajili ya kuweka sawa haki ya wale wenye kuuziana, ama kipimo wakati wa kutoa sadaka haipendezi (si katika sunna).

Marejeo

كنوز رياض الصالحين، أ.د. حمد بن ناصر بن عبد الرحمن العمار، دار كنوز إشبيليا، الطبعة الأولى: 1430 هـ. بهجة الناظرين، الشيخ: سليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي. نزهة المتقين، د. مصطفى سعيد الخن، د. مصطفى البغا، محيي الدين مستو، علي الشرجبي، محمد أمين لطفي، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة الأولى: 1397 هـ 1977 م، الطبعة الرابعة عشرة 1407 هـ 1987م. شرح صحيح البخاري لابن بطال، المؤلف: ابن بطال أبو الحسن علي بن خلف بن عبد الملك، تحقيق: أبو تميم ياسر بن إبراهيم، دار النشر: مكتبة الرشد - السعودية، الرياض، الطبعة: الثانية، 1423هـ - 2003م. رياض الصالحين، د. ماهر بن ياسين الفحل، الناشر: دار ابن كثير للطباعة والنشر والتوزيع، دمشق - بيروت، الطبعة: الأولى، 1428 هـ - 2007 م. صحيح مسلم، المؤلف: مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، المحقق: محمد فؤاد عبد الباقي، الناشر: دار إحياء التراث العربي - بيروت. صحيح البخاري، المؤلف: محمد بن إسماعيل أبو عبدالله البخاري الجعفي، المحقق: محمد زهير بن ناصر الناصر، الناشر: دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422هـ. المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، المؤلف: أبو زكريا محيي الدين يحيى بن شرف النووي، الناشر: دار إحياء التراث العربي - بيروت، الطبعة: الثانية، 1392.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «كُلُّ أُمَّتِي يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَنْ أَبَى»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، وَمَنْ يَأْبَى؟ قَالَ: «مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أَبَى».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni nani atakaye kataa? Akasema: "Atakaye nitii ataingia peponi, na atakaye niasi atakuwa amekataa".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba umma wake wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa!. Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- wakasema: Ni nani atakaye kataa ewe Mjumbe wa Allah?! Akawajibu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa atakayejisalimisha na akafuata na akamtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ataingia peponi, na ama atakaye asi na akawa hakujisalimisha katika sheria atakuwa kakataa mwenyewe kuingia peponi kwa sababu ya matendo yake mabaya.

Mafunzo
  1. Nikuwa kumtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kumuasi kwake ni sehemu ya kumuasi Mwenyezi Mungu.
  2. Kumtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hupelekea kuipata pepo, na kumuasi kwake kunapelekea kuingia motoni.
  3. Habari njema kwa watiifu walioko katika umma huu, nakuwa wote wataingia peponi isipokuwa atakayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
  4. Huruma yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa umma wake, na pupa yake katika kuwaongoa.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 92) (7280). فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي، المكتبة التجارية الكبرى – مصر، الطبعة: الأولى. بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين لسليم الهلالي، ط1، دار ابن الجوزي، الدمام، 1415هـ. التيسير بشرح الجامع الصغير، للمناوي، مكتبة الإمام الشافعي، الرياض، ط3.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَيُوشِكَنَّ أَنْ يَنْزِلَ فِيكُمْ ابْنُ مَرْيَمَ حَكَمًا مُقْسِطًا، فَيَكْسِرَ الصَّلِيبَ، وَيَقْتُلَ الخِنْزِيرَ، وَيَضَعَ الجِزْيَةَ، وَيَفِيضَ المَالُ حَتَّى لاَ يَقْبَلَهُ أَحَدٌ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya ukaribu wa kuteremka Issa mwana wa Mariam amani iwe juu yake ili ahukumu baina ya watu kwa uadilifu na kwa sheria ya Muhammadi. nakuwa atavunja misalaba wanayoitukuza wakristo, nakuwa Issa amani iwe juu yake ataua nguruwe, Na pia amani iwe juu yake ataweka kodi (Jizia) na atawaamrisha watu wote kuingia katika Uislamu. Nakuwa mali itaenea na hatoikubali yeyote; na hii ni kwa sababu ya wingi wake, na kwa kutosheka kila mmoja na kile anachokimiliki mkononi mwake, na kuteremka kwa baraka na heri nyingi zenye kufuatana.

Mafunzo
  1. Kumethibitishwa kuteremka kwa Issa amani iwe juu yake zama za mwisho, nakuwa tukio hilo ni katika alama za Kiyama.
  2. Sheria ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haitofutwa na sheria yoyote.
  3. Kuteremka kwa baraka katika mali zama za mwisho, na watu kutoipenda.
  4. Habari njema ya kubakia kwa dini ya Uislamu kiasi ambacho Issa amani iwe juu yake atawahukumu watu zama za mwisho.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 82) (2222)، صحيح مسلم (1/ 135) (155)، شرح النووي على مسلم (1/471)، التوضيح (14/555)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (12/ 35).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

na mimi ndiye ninaitwa Dhwamam Bin Thaalaba ndugu wa Banii Saad Bin Bakri

عن أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ رضي الله عنه قال: بينما نحن جلوس مع النبي صلى الله عليه وسلم في المسجد دخل رجل على جمل، فأناخه في المسجد ثم عقله، ثم قال لهم: أيكم محمد؟ والنبي صلى الله عليه وسلم متكئ بين ظهرانيهم، فقلنا: هذا الرجل الأبيض المتكئ. فقال له الرجل: يا ابن عبد المطلب فقال له النبي صلى الله عليه وسلم: «قد أجبتك». فقال الرجل للنبي صلى الله عليه وسلم: إني سائلك فمشدد عليك في المسألة، فلا تجد علي في نفسك؟ فقال: «سل عما بدا لك» فقال: أسألك بربك ورب من قبلك، آلله أرسلك إلى الناس كلهم؟ فقال: «اللهم نعم». قال: أنشدك بالله، آلله أمرك أن نصلي الصلوات الخمس في اليوم والليلة؟ قال: «اللهم نعم». قال: أنشدك بالله، آلله أمرك أن نصوم هذا الشهر من السنة؟ قال: «اللهم نعم». قال: أنشدك بالله، آلله أمرك أن تأخذ هذه الصدقة من أغنيائنا فتقسمها على فقرائنا؟ فقال النبي صلى الله عليه وسلم: «اللهم نعم». فقال الرجل: آمنت بما جئت به، وأنا رسول من ورائي من قومي، وأنا ضمام بن ثعلبة أخو بني سعد بن بكر.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Wakati mmoja tulipokuwa tumekaa Msikitini pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliingia mtu mmoja akiwa juu ya Ngamia, akampigisha magoti Ngamia ndani ya Msikiti kisha akamfunga, kisha akawaambia Maswahaba: Kati yenu Muhammad ni nani? Na wakati huo Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake- akiwa kati yao amekaa kwa kuegemea, tukasema ni huyu mtu mweupe aliyeegemea, yule mtu akamwambia: Ewe mtoto wa Abdul Muttwalib, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: "Nimekuitikia" Yule bwana akamwambia Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- Hakika mimi nitakuuliza nanitatia mkazo katika kuuliza, hivyo usinichukie kwenye moyo wako, na wala usiona tabu kunijibu, akasema: "Uliza unachotaka" Akasema: Nanakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa waliokuwa kabla yako, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote? Akasema: "Ndiyo, ni kweli" Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu ametuamrisha sisi tusali sala tano usiku na mchana? Akasema:"Ndiyo, ni kweli" Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa sisi tufunge Mwezi huu kila Mwaka? Akasema: "Ndiyo, ni kweli" Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa uchukue hizi sadaka kutoka kwa matajiri na uzigawanye kwa mafukara wetu? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ndiyo, ni kweli" Basi yule bwana akasema: Nimeamini yote yale uliyokuja nayo, na mimi ni mjumbe kuna wanaonifuata nyuma yangu, na mimi ndiye ninaitwa Dhwamam Bin Thaalaba ndugu wa Banii Saad Bin Bakri."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anatoa habari Anas Bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Wakati mmoja Maswahaba walikuwa wamekaa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Msikitini aliingia mtu mmoja akiwa juu ya Ngamia, basi akampigisha magoti kisha akamfunga Ngamia wake, Kisha akawauliza: Kati yenu Muhammad ni nani? Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa amekaa kati ya watu na ameegemea, tukamwambia: Ni mtu huyu mweupe aliyeegemea, Yule bwana akamwambia: Ewe mtoto wa Abdul Muttwalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nimekusikia, basi uliza nitakujibu. Yule bwana akamwambia Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake-: Mimi nitakuuliza na nitakuuliza kwa msisitizo mkubwa hivyo usinichukie wala usione dhiki katika nafsi yako. Yaani: Usinikasirikie wala usione dhiki, Akasema: Uliza unachotaka, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa waliokuwa kabla yako, Je ni kweli Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote? Akasema: Ndiyo ni kweli, hali ya kutilia mkazo ukweli wake, Yule bwana akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha yakuwa sisi tusali sala tano usiku na mchana? Nazo ni sala za faradhi, Akasema: Ndiyo ni kweli, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha yakuwa sisi tuufunge Mwezi huu katika kila Mwaka? Yaani Mwezi wa Ramadhan, Akasema: Ndiyo ni kweli, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa uchukue hizi sadaka kutoka kwa matajiri wetu kisha uzigawe kwa mafukara wetu? Na sadaka hiyo ni Zaka, Basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-Ndiyo ni kweli, Basi Dhwamamu akasilimu, na akamwambia Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atawalingania watu wake kuingia kwenye uislamu, kisha akajitambulisha kuwa yeye ni Dhwammam Bin Thaalabah atokanae na kabila la Banii Saad Bin Bakri.

Mafunzo
  1. Unyenyekevu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa namna ambayo hakuweza mtu yule kumtofautisha kati ya Mtume na Maswahaba zake.
  2. Uzuri wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- upole wake katika kumjibu muulizaji, na kuwa kurudisha majibu mazuri ni miongoni mwa sababu ya kukubalika Daawa.
  3. Inafaa mtu kujitambulisha kwa sifa ya rangi ya weupe au wekundu, na urefu na ufupi, na mfano wa sifa hizo ikiwa haikusudiwi kuaibisha, ikiwa msifiwa hatochukia sifa hizo.
  4. Yafaa kwa Kafiri kuingia Msikitini kwa haja maalumu.
  5. Haikutajwa Hijja katika hadithi kwa sababu hueda ikawa Hijja ilikuwa haijafaradhishwa wakati wakuja kwake.
  6. Pupa ya Maswahaba ya kuwalingania watu; Basi kwa muda mfupi tu baada ya kusilimu kwake alikuwa na pupa ya kuwalingania watu wake.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 23) (63)، صحيح مسلم (1/ 41) (12)، شرح ابن بطال (1/145)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (2/ 22).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 12
Hadithi 12
  1. Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hatonisikia yeyote katika umma huu, Myahudi wala Mkristo, kisha akafa haliyakuwa hajayaamini yale niliyotumwa kwayo, isipokuwa atakuwa ni katika watu wa motoni
  2. Tukasema: Wewe ni bwana yetu, akasema: "Bwana ni Mwenyezi Mungu", Tukasema: Na mbora zaidi kuliko sisi katika fadhila, na mtoaji zaidi kuliko sisi, akasema: "Semeni kwa maneno mliyozoea, au baadhi yake, na wala asikukokoteni Shetani
  3. Nyanyua kichwa chako na sema yasikilizwe, na omba upewe, na taka utetezi utetewe
  4. Nimepewa mambo matano ambavyo hakupewa mtu mwingine miongoni mwa Manabii kabla yangu
  5. Alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa hakuna chochote nyumbani kwake anachoweza kukila mwenye ini (uhai) ila kiasi kidogo cha ngano kilichokuwa katika ubao wangu (wa kuhifadhia chakula), nikala mpaka kikakaa muda mrefu, nilipokipima kikamalizika
  6. Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa
  7. Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hivi karibuni atakuteremkieni Issa mwana wa Mariam atakuwa hakimu na muadilifu, atavunja misalaba, na ataua nguruwe, na ataweka kodi (Jizia), na mali itabugujika (itakuwa nyingi) mpaka itafikia mahali hakuna yeyote atakayeikubali
  8. na mimi ndiye ninaitwa Dhwamam Bin Thaalaba ndugu wa Banii Saad Bin Bakri
  9. Uliteremshwa Wahyi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka arobaini
  10. Andika, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakitoki ndani yake ila haki
  11. Hakika mchamungu wenu na mwenye kumjua zaidi Mwenyezi Mungu kwenu nyinyi ni mimi
  12. Hakuna yeyote katika Manabii isipokuwa alipewa mfano wa yale waliyoyaamini watu

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com