Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Mwenyezi Mungu amempa mambo matano ambayo hakupewa yeyote katika Manabiii kabla yake: La kwanza: Nimeepushwa na hofu, na hofu hiyo inatiwa katika nyoyo za maadui zangu hata kukiwa kati yangu na wao mwendo wa kutembea mwezi mzima. La pili: Tumefanyiwa Ardhi kwetu kuwa Msikiti tuswali mahala popote tutakapokuwa, na udongo wake ni twahara (safi) pale tunaposhindwa kutumia maji. La tatu: Tumehalalishiwa ngawira za vita, nazo ni zile wanazozichukua waislamu katika vita vyao na makafiri. La nne: Nimepewa utetezi mkubwa katika kuwapumzisha watu na misukosuko ya kisimamo cha siku ya Kiyama. La tano: Nimetumwa kuja kwa viumbe wote binadam wao na majini wao, kinyume na Manabii walikokuwa kabla yake, walikuwa wakitumwa kwa watu wao pekee.
- Sheria ya mtu kuhesabu neema za Mwenyezi Mungu juu yake kwa kuzisimulia na kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizo.
- Fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya umma huu na kwa Nabii wao, kwa kupewa mambo haya.
- Uwajibu wa kuitekeleza swala kwa wakati wake kwa hali yoyote ile itakayokuwa, na mtu afanye awezacho katika sharti zake na nguzo zake na wajibu wake.
- Utetezi maalumu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake unaotofautiana na wa Manabii, una aina nyingi: Ya kwanza: Utetezi wake kwa viumbe ili hukumu ipite baina yao, na pia: Utetezi wake wa kuingia watu wa peponi peponi, na pia: Utetezi wake maalumu kwa ami yake Abii Twalib katika kupunguziwa adhabu ya moto si kutolewa kwenye moto; kwa sababu alikufa kafiri.
- Mambo ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni mengi mno ambayo hayakutajwa katika hadithi hii yakiwemo: Alipewa mkusanyo wa maneno (maneno machache yenye maana pana), na umehitimishwa utume kupitia kwake, na zimefanywa safu zetu kuwa kama safu za Malaika, na mambo mengine mengi.
صحيح البخاري (1/ 74) (335). صحيح مسلم (1/ 370) (521). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص74). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 94).