Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «كُلُّ أُمَّتِي يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ إِلَّا مَنْ أَبَى»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، وَمَنْ يَأْبَى؟ قَالَ: «مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أَبَى».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Umma wangu wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni nani atakaye kataa? Akasema: "Atakaye nitii ataingia peponi, na atakaye niasi atakuwa amekataa".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba umma wake wote wataingia peponi isipokuwa atakaye kataa!. Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- wakasema: Ni nani atakaye kataa ewe Mjumbe wa Allah?! Akawajibu -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa atakayejisalimisha na akafuata na akamtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ataingia peponi, na ama atakaye asi na akawa hakujisalimisha katika sheria atakuwa kakataa mwenyewe kuingia peponi kwa sababu ya matendo yake mabaya.

Mafunzo
  1. Nikuwa kumtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kumuasi kwake ni sehemu ya kumuasi Mwenyezi Mungu.
  2. Kumtii Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hupelekea kuipata pepo, na kumuasi kwake kunapelekea kuingia motoni.
  3. Habari njema kwa watiifu walioko katika umma huu, nakuwa wote wataingia peponi isipokuwa atakayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
  4. Huruma yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa umma wake, na pupa yake katika kuwaongoa.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 92) (7280). فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي، المكتبة التجارية الكبرى – مصر، الطبعة: الأولى. بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين لسليم الهلالي، ط1، دار ابن الجوزي، الدمام، 1415هـ. التيسير بشرح الجامع الصغير، للمناوي، مكتبة الإمام الشافعي، الرياض، ط3.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Mtume wetu Muhammad - Rehema na amani za Allah ziwe juu yake-

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com