Imepokelewa kutoka kwa Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anawaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wenye kuswali kunyoosha safu zao, na wasitanguliane wala wasirudi nyuma, na kwamba kuzinyoosha ni sehemu ya kukamilisha na ukamilifu wa Sala, na kuwa kupinda kwa safu ni dosari na ni upungufu ndani yake.
Mafunzo
Sheria ya kuchunga kila kinachokamilisha swala na kuiweka mbali na upungufu.
Hekima ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kufundisha, kwani aliihusisha hukumu na sababu yake; ili iwe wazi hekima ya kuletwa sheria hiyo, na nafsi ipate hamasa ya kuitekeleza.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 145) (723).
صحيح مسلم (1/ 324) (433).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص127).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 161).
الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص173).
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم: «اللهُمَّ لَا تَجْعَلْ قَبْرِي وَثَنًا، لَعَنَ اللهُ قَوْمًا اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Ewe Mwenyezi Mungu, usilifanye kaburi langu kuwa ni sanamu, Allah amewalaani watu walioyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti".
Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mola wake asilifanye kaburi lake kuwa mithili ya sanamu lenye kuabudiwa na watu kwa kulitukuza, na kulielekea wakati wa kusujudu; kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi mungu yuko mbali na amemumfukuza na kumtowa kwenye rehema zake yeyote atakaye fanya makaburi ya manabii kuwa ni misikiti,kwani kulifanya kuwa msikiti ni njia ya kuelekea kuliabudu na kuliitakidi hivyo.
Mafunzo
Kuvuka mpaka wa kisheria katika makaburi ya Manabii na watu wema hufanya yaabudiwe kinyume na Mwenyezi Mungu, ni lazima kuchukua tahadhari na njia zinazopelekea katika ushirikina.
Haifai kwenda makaburini kwa lengo la kuyatukuza na kufanya ibada hapo, vyovyote vile utakavyokuwa ukaribu wa mwenye kaburi na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Uharamu wa kujenga misikiti juu ya makaburi.
Uharamu wa kuswali makaburini hata kama hujajengwa msikiti hapo, isipokuwa swala ya jeneza ambalo halijaswaliwa (wanaweza kuswalia kwa dharura hiyo)
Marejeo
مسند أحمد (12/ 314) (7358).
فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، لعبد الرحمن التميمي (1/ 434).
القول المفيد على كتاب التوحيد، لمحمد بن عثيمين (1/ 434).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص178).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص194).
التمهيد لشرح كتاب التوحيد، لصالح آل الشيخ (ص51).
مشكاة المصابيح، للتبريزي (1/ 234).
عن علي بن الحسين: "أنه رأى رجلا يجيء إلى فُرْجَةٍ كانت عند قبر النبي صلى الله عليه وسلم فيدخل فيها فيدعو، فنهاه، وقال: ألا أحدثكم حديثا سمعته من أبي عن جدي عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:« لا تتخذوا قبري عيدا، ولا بيوتكم قبورا، وصلوا علي، فإن تسليمكم يبلغني أين كنتم».
Kutoka kwa Ally bin Husein: "Yakwamba yeye aliona mtu mmoja anakuja toka katika kiupenyo kidogo kilikuwa katika kaburi la Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anaingia na anaomba hapo, akamkataza, na akasema: Hivi nikusimulieni hadithi niliyoisikia toka kwa baba yangu toka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- amesema: "Msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, wala nyumba zenu kuwa makaburi, na nitakieni rehma, kwani dua zenu hunifikia popote mlipo".
Imepokelewa na Ibn Abii ShaybahDarajaNi sahihi kwa njia zake na ushahidi wake
Maelezo
Anatueleza Ally bin Husein -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba yeye alimuona mtu mmoja akimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu katika kaburi la Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-, nakuwa yeye alimkataza juu ya hilo kwa ushahidi wa hadithi ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ambayo limekuja ndani yake katazo la kulifanyia mazoea kaburi lake kwa ziara, na katazo la kuzitelekeza nyumba kwa kutokuwa na ibada ya Mwenyezi Mungu ndani yake na dhikri, na kuifananisha kwake na kaburi, na akaeleza kuwa salamu ya muislamu itamfikia yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- mahala popote atakapokuwa muislamu.
Marejeo
كتاب التوحيد، للإمام محمد بن عبد الوهاب، ت: د. دغش العجمي، مكتبة أهل الأثر, الطبعة الخامسة, 1435ه.
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد بن عبد العزيز السليمان القرعاوي, ت: محمد بن أحمد سيد, مكتبة السوادي، الطبعة: الخامسة، 1424ه.
الملخص في شرح كتاب التوحيد، للشيخ صالح الفوزان, دار العاصمة, الطبعة الأولى، 1422ه.
مصنف ابن أبي شيبة، تحقيق: كمال يوسف الحوت، نشر: مكتبة الرشد - الرياض، الطبعة: الأولى، 1409ه.
تحذير الساجد من اتخاذ القبور مساجد, الألباني, المكتب الإسلامي - الطبعة: الرابعة.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Miji inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake, na miji inayochukiwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sehemu zinazopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni misikiti yake; kwa sababu ni nyumba za ibada, na zimeasisiwa kwa uchamungu, na miji inayochukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni masoko yake; kwa sababu masoko mara nyingi ndio kitovu cha ghushi na udanganyifu na riba na viapo vya uongo, na kwenda kinyume na ahadi, na kupuuza kumtaja Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Utukufu wa misikiti na heshima yake; kwa sababu ni nyumba ambazo hutajwa ndani yake jina la Mwenyezi Mungu kwa wingi.
Himizo la kudumu kuwa msikitini, na wingi kwenda ndani yake, kwa kutafuta mapenzi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na radhi zake, na kupunguza kuzunguka masokoni, isipokuwa kwa haja maalumu; kwa kujiepusha kuingia katika sababu za hasira ya Mwenyezi Mungu.
Amesema Nawawi: Misikiti ni mahali pa kushuka rehema na masoko ni kinyume chake.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 464) (671).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1250).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 305).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 655).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (21/ 526).
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Siku moja sisi tukiwa Msikitini pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake ghafla akaja bedui, akasimama akaanza kukojoa Msikitini, wakasema Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Koma, koma!, anasema: Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Msimkatishe, muacheni" Wakamuacha mpaka akamaliza kukojoa, kisha baada ya hapo Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuita, akasema kumuambia: "Hakika Misikiti hii haifai kuwekwa chochote katika mikojo hii, wala uchafu wowote, bali hii ni kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuswali, na kusoma Qur'ani" Au kama alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema; akumuamrisha mtu mmoja miongoni mwao akaja na ndoo ya maji akapamwagia.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake msikitini kwake akiwa pamoja na Maswahaba zake, akaja bedui mmoja kutoka kijijini, akaanza kukojoa katika kona ya msikiti. Maswahaba wakamkaripia na wakasema: Koma, na wacha unachokifanya. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Muacheni, na wala msimkatishe mkojo wake, wakamuacha mpaka akamaliza.
Kisha rehema na amani ziwe juu yake akamuita na akamwambia: Hakika misikiti haifai kwa chochote miongoni mwa mikojo hii, wala aina yoyote ya uchafu, bali ni kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na swala, na kusoma Qur'ani na mfano wa hayo. Kisha akamuamrisha rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja katika Maswahaba akaja na ndoo iliyojaa maji akayamwaga katika mkojo wake.
Mafunzo
Uwajibu wa kuitukuza misikiti, na kuilinda na yale yasiyofaa.
Amesema Nawawi: Hapa kuna kuilinda misikiti na kuitakasa kutokana na uchafu na takataka na mate, na kunyanyua sauti na ugomvi, na kuuuza na kununua, na mikataba yote, na yenye kufanana na hayo.
Kumuhurumia mjinga na kumfundisha yanayompasa bila kumkaripia wala kumuudhi ikiwa hatofanya kosa kwa kudharau au makusudi.
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni mwalimu mpole, na muadabishaji mwenye huruma, na mlezi mwenye huruma.
Himizo la kuziimarisha nyumba za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa swala na Qur'ani na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 54) (221).
صحيح مسلم (1/ 236) (285).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1159).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (20/ 98).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 191).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 436).
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mama Salama alimsimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kisa cha kanisa aliloliona katika ardhi ya Ethiopia, likiitwa kanisa la Mtakatifu Maria, akasimulia aliyoyaona ndani yake miongoni mwa picha, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Watu hao anapokufa kwao mja mwema, au mwanaume mwema, wanajenga juu ya kaburi lake mahala pakuabudia, na wanachora ndani yake picha hizo, hao ndio viumbe waovu zaidi mbele ya Allah
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amesimulia mama wa waumini mama Salama radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba alipokuwa katika ardhi ya Ethiopia aliona Kanisa -linaloitwa kwa jina la Mtakatifu Maria- ndani yake kukiwa na picha na mapambo na michoro; akastaajabu kwa kitendo hicho!. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akafafanua sababu za kuwekwa picha hizo; Akasema: Hakika hao unaowataja hapa walikuwa anapokufa kwao mtu mwema wanajenga Msikiti juu ya kaburi lake, na wanasali ndani yake, na wanachoro picha hizo, Na akabainisha kuwa mfanyaji wa hilo ni kiumbe muovu zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu kitendo chake hicho kinapelekea katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mafunzo
Uharamu wa kujenga Misikiti juu ya makaburi, au kuswali hapo, au kuzika maiti ndani ya msikiti; hii ikiwa ni kuziba njia za kuelekea katika ushirikina.
Kujenga Misikiti juu ya makaburi, na kutundika picha, hiki ni kitendo cha Mayahudi, nakuwa mwenye kufanya hivi atakuwa kafanana nao.
Uharamu wa kutengeneza picha za viumbe hai (wenye roho).
Atakayejenga msikiti juu ya kaburi na akachoro ndani yake picha, huyu ni katika viumbe waovu zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Sheria imeuhami sana upande wa tauhidi kwa himaya iliyokamilika, kwa kuziba njia zote ambazo zinaweza kusababisha kufika katika ushirikina.
Katazo la kuchupa mipaka kwa watu wema; kwani ni sababu ya kuingia katika shirki.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 94) (434).
صحيح مسلم (1/ 375) (528).
مرقاة المفاتيح، لعلي القاري (7/ 2857).
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 115).
فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 598).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (2/ 469).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص290).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص183).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص168).
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- Ya kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakitosimama Kiyama mpaka watu wajifaharishe katika Misikiti".
Imepoekelewa na Abu Daud, Nasai na Ibn MajahDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa miongoni mwa dalili za kukaribia kwa Kiyama na kumalizika kwa Dunia, ni watu kujifaharisha kwa kuipamba Misikiti yao, au kujifaharisha kwa dunia yao ndani ya misikiti ambayo haikujengwa ila kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Uharamu wa kujifaharisha kwa Misikiti, na kwamba ni jambo lisilokubalika; kwa sababu kitendo hicho hakikufanyika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Katazo la kuipamba Misikiti kwa rangi na vito na nakshi, na maandishi; kwa sababu ndani yake kuna kuwashughulisha wenye kuswali wanapoyatazama.
Amesema Assanadi: Hadithi ni miongoni mwa zile ambazo uhalisia unashuhudia yaliyosemwa, ni miongoni mwa miujiza ya kushangaza ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Marejeo
سنن أبي داود (1/ 337) (449).
سنن النسائي (2/ 32) (689).
سنن ابن ماجه (1/ 475) (739)،.
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 137).
فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 621).
Kutoka kwa Mahmud bin Labidi radhi za Allah ziwe juu yake: Anasimulia kuwa Othman bin Affan alitaka kujenga msikiti watu hawakulipenda swala hilo, na wakapendelea auache katika muonekano wake, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayejenga msikiti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu atamjengea Peponi nyumba mfano wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Othman bin Affan alitaka kuujenga msikiti wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa sura nzuri zaidi kuliko jengo lake la awali, watu hawakupendezwa na swala hilo; kwa sababu msikiti utabadilika kutoka katika muonekano wa jengo lake lilivyokuwa katika zama za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, msikiti ulikuwa umejengwa kwa matofali, na paa lake lilikuwa limeezekwa kwa makuti, lakini Othman alitaka kuujenga kwa mawe na chokaa, Othman radhi za Allah ziwe juu yake akawaeleza kuwa yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Atakayejenga msikiti kwa kutafuta radhi zake Mtukufu, si kwa kutaka kujionyesha au kusikika, Mwenyezi Mungu atamlipa malipo bora kulingana na amali yake, na malipo hayo ni Mwenezi Mungu kumjengea mfano wake peponi.
Mafunzo
Himizo la kujenga misikiti na fadhila zake.
Kupanua msikiti na kuukarabati yote haya yanaingia katika fadhila za kujenga.
Umuhimu wa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 97) (450)، صحيح مسلم (4/ 2287) (533)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (2/ 131)، شرح النّووي على مسلم (5/14)، التوضيح لشرح الجامع الصحيح (5/537)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (12/ 171).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com