عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَا يَزَالُ البَلاَءُ بِالمُؤْمِنِ وَالمُؤْمِنَةِ فِي نَفْسِهِ وَوَلَدِهِ وَمَالِهِ حَتَّى يَلْقَى اللَّهَ وَمَا عَلَيْهِ خَطِيئَةٌ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Majaribio hayaachi kumpata muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake, na watoto wake, na mali yake mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu ilhali hana dhambi hata moja."
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa: “Balaa na mtihani havikomi kwa muumini wa kiume na wa kike, katika afya yake na mwili wake, na kwa watoto wake, kama magonjwa, kifo, uasi na mengineyo, na katika mali yake kutiwa umasikini, kutoweka kwa biashara, kuibiwa, kuvurugika kwa maisha na dhiki katika riziki, na ugumu wa maisha, mpaka Mwenyezi Mungu atamfutia dhambi zake zote kwa mateso haya, ili atakapokutana na Mwenyezi Mungu atakuwa kasafishika na madhambi na maovu yote aliyoyafanya.
Mafunzo
- Miongoni mwa huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake waumini ni kuwafutia madhambi yao katika dunia yao kupitia matatizo ya dunia na maafa yake.
- Balaa pekee linafuta madhambi ila kwa sharti la imani, hivyo akisubiri mja na akawa hakulalamika basi analipwa.
- Himizo la subira katika mambo yote, katika yale ayapendayo na anayoyachukia, awe na subira mpaka atekeleze aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu, na awe na subira mpaka akae mbali na yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu, akitaraji malipo ya Mwenyezi Mungu na kuogopa adhabu yake.
- Kauli yake: “Kwa muumini mwanaume na mwanamke,” kuongeza neno “muumini wa kike” ndani yake ni ushahidi wa kutiliwa mkazo zaidi kwa wanawake. Vinginevyo, lau angesema: "Kwa muumini wa kiume," mwanamke angejumuishwa ndani yake; Kwa sababu hii si mahsusi kwa wanaume, basi ikiwa dhiki itampata mwanamke, naye anaahidiwa malipo kama hayo kwa kufutiwa madhambi na makosa.
- Hili ni miongoni mwa mambo yanayomtia faraja mtu kwa yale anayokumbana nayo katika maumivu kila mara yanayosababishwa na mabalaa.
Marejeo
سنن الترمذي (4/ 204) (2399).
مسند أحمد (13/ 248) (7859).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 113).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص51).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 273).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 80).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضيَ اللهُ عنهما: أنَّهُ قَالَ لعَطَاءِ بْنِ أَبِي رَبَاحٍ: أَلَا أُرِيكَ امْرَأَةً مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ؟ قُلْتُ: بَلَى، قَالَ: هَذِهِ الْمَرْأَةُ السَّوْدَاءُ، أَتَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: إِنِّي أُصْرَعُ وَإِنِّي أَتَكَشَّفُ، فَادْعُ اللهَ لِي، قَالَ: «إِنْ شِئْتِ صَبَرْتِ وَلَكِ الْجَنَّةُ، وَإِنْ شِئْتِ دَعَوْتُ اللهَ أَنْ يُعَافِيَكِ» قَالَتْ: أَصْبِرُ، قَالَتْ: فَإِنِّي أَتَكَشَّفُ فَادْعُ اللهَ أَنْ لَا أَتَكَشَّفَ، فَدَعَا لَهَا.
Kutoka kwa bin Abbasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yeye na baba yake: Ya kwamba pindi aliposema kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Hivi je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa wanawake wa Peponi? Nikasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika mimi huanguka, na nguo zangu hufunuka ninapoanguka, nakuomba uniombee kwa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye" Akasema: Bali nitavumilia, akasema: Lakini mimi huwa nafunuka nguo, basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke, basi akamuombea.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alisema bin Abbasi Mwenyezi Mungu amuwie radhi kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa watu wa Peponi? Atwaa akasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke muethiopia mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: akasema: Hakika mimi nina maradhi, huanguka na kufunuka nguo zangu, na kuonekana sehemu ya mwili wangu pasina mimi kujielewa, basi muombe Mwenyezi Mungu aniponye, akasema: Ukipenda unaweza kuvumilia na utakuwa na malipo ya Pepo, na ukipenda nitamuomba Mwenyezi Mungu akuponye, akasema: Basi nitavumilia, kisha akasema: Basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke nikianguka, basi akamuombea kwa Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
- Subira juu ya mabalaa katika dunia hupelekea kupata Pepo.
- Amesema Nawawi: Na hapa kuna ushahidi kuwa ugonjwa wa kuanguka kwa mtu hulipwa malipo yaliyokamilika
- Tazama heshima na haya kwa wanawake wa kiswahaba, na pupa yao juu ya kujisitiri, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, mwanamke huyu, kubwa zaidi alilokuwa akilihofia ni kufunuka sehemu ya mwili wake.
- Amesema bin Hajari: Kuchukua jambo gumu ni bora kuliko kuchukua ruhusa, kwa mtu atakayejua kuwa anauwezo wa kulibeba, na hatodhoofika kwa kulibeba gumu hilo.
- Amesema bin Hajari: Na hapa nikuwa; tiba ya maradhi yote ni kwa dua na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, hufaa zaidi na kunufaisha zaidi kuliko tiba ya miti shamba (madawa), na kwamba athari ya hilo na muitikio wa mwili ni mkubwa zaidi kuliko athari ya dawa za mwili, lakini huleta ahueni kwa mambo mawili: La kwanza: Upande wa mgonjwa, kuwa na imani ya kweli na Mwenyezi Mungu, na la pili: Upande wa tabibu, kuwa na nguvu kubwa ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa na nguvu kubwa ya uchamungu, na kumtegemea Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi zaidi.
- Amesema bin Hajari: Hapa kuna ushahidi juu ya kuacha kutumia dawa.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 116) (5652).
صحيح مسلم (4/ 1994) (2576).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 95).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 235).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: "إن عِظَمَ الجزاءِ مع عِظَمِ البلاءِ، وإن الله تعالى إذا أحب قوما ابتلاهم، فمن رَضِيَ فله الرِضا، ومن سَخِطَ فله السُّخْطُ".
Kutoka kwa Anas bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, yakuwa yeye Amesema: "Hakika ukubwa wa malipo huendana sawa pamoja na ukubwa wa matatizo, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapowapenda watu huwapa mtihani; atakayeridhia atapata radhi, na atakayechukia atapata hasira (za Mwenyezi Mungu)."
Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo
Anatueleza Mtume rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi kuwa muumini linaweza kutokea kwake jambo lolote katika matatizo, katika nafsi yake au mali yake au kinginecho, nakuwa Mwenyezi Mungu atamlipa juu ya matatizo hayo ikiwa kama yeye atavumilia, nakuwa kila majanga yanavyozidi kuwa makubwa na hatari yake kuwa kubwa ndivyo malipo yake yanavyokuwa makubwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha anabainisha rehema na Amani zimfikie kuwa mitihani ni katika alama za kuwapenda Mwenyezi Mungu waumini, nakuwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake ni lazima yafanyike hakuna namna, lakini atakayesubiri na akaridhia, basi Mwenyezi Mungu atamlipa kwa hilo kwa kumridhia na zinamtosha zaidi thawabu zake, nakuwa atakayechukia na akakerwa na hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake, basi Mwenyezi Mungu atamchukia na zinamtosha zaidi adhabu zake.
Mafunzo
- Nikuwa matatizo yanafuta madhambi, madam tu hajaambatana na kuacha la wajibu, kama kuacha kuvumilia, au kufanya la haramu kama kuchana nguo na kupiga mashavu.
- Kuthibitisha sifa ya mapenzi kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inayoendana na Utukufu wake.
- Hakika matatizo kwa Muumini ni katika alama za Imani.
- Kuthibitisha sifa ya kuridhia na kuchukia kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inayoendana na Utukufu wake.
- Kupendeza kuridhika na hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake.
- kuharamishwa kukasirikia hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake.
- Kuhimizwa kuvumilia juu ya matatizo.
- Mwanadamu anaweza kuchukia jambo nalo likawa na kheri.
- Kuthibitisha hekima kwa Mwenyezi Mungu katika vitendo vyake.
- Malipo huendana na matendo.
Marejeo
كتاب التوحيد للإمام محمد بن عبد الوهاب، ت: د. دغش العجمي، مكتبة أهل الأثر, الطبعة الخامسة, 1435ه.
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد بن عبد العزيز السليمان القرعاوي, ت: محمد بن أحمد سيد, مكتبة السوادي، الطبعة: الخامسة، 1424ه.
الملخص في شرح كتاب التوحيد، دار العاصمة، الرياض، الطبعة: الأولى 1422هـ - 2001م.
جامع الترمذي، ت: أحمد شاكر, شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي, الطبعة: الثانية، 1395هـ.
صحيح الجامع الصغير , للألباني , المكتب الإسلامي.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ طَاوُسٍ أَنَّهُ قَالَ: أَدْرَكْتُ نَاسًا مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُونَ كُلُّ شَيْءٍ بِقَدَرٍ، قَالَ: وَسَمِعْتُ عَبْدَ اللهِ بْنَ عُمَرَ رضي الله عنهما يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «كُلُّ شَيْءٍ بِقَدَرٍ، حَتَّى الْعَجْزِ وَالْكَيْسِ، أَوِ الْكَيْسِ وَالْعَجْزِ».
Imepokelewa kutoka kwa Twaausi kuwa yeye amesema: Niliwakuta watu miongoni mwa maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- wakisema kuwa kila kitu huwa kwa namna ilivyopangwa, akasema: Na nimemsikia Abdullah bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake- anasema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kila jambo linakuwa kwa namna lilivyopangwa, mpaka kushindwa kufanya jambo fulani au kulifanya kwa ufanisi, au kufanya kwa ufanisi au kushindwa kabisa kufanya."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila jambo linakuwa kwa mujibu wa lilivyopangwa; Mpaka kushindwa: Nako nikuacha jambo ambalo ni wajibu kulifanya au kulichelewesha katika mambo ya kidunia au ya Akhera. Na hata kufanya jambo kwa ufanisi: Nako ni kufanya kwa uchangamfu na weledi katika mambo ya kidunia au ya Akhera. Na hakika Mwenyezi Mungu amepangilia jambo la kushindwa au kufanya kwa ufanisi na amepangilia kila kitu, hakuna chochote kinachotokea isipokuwa kinatokea kwa ujuzi wake Mwenyezi Mungu na kutaka kwake.
Mafunzo
- Imewekwa wazi itikadi ya Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika kuamini mipango ya Mwenyezi Mungu -Kadari-.
- Kila kitu kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu mpaka kushindwa na kuweza kufanya jambo.
- Uimara wa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika kupokea na kufikisha maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake.
- Kuamini -Kadari- kheri zake na shari zake.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2045) (2655)، إكمال المعلم (8/143)، شرح النووي على مسلم (16/205)، الفتح الرباني لترتيب مسند الإمام أحمد بن حنبل الشيباني (1/ 122).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ مَطَرِ بْنِ عُكَامِسٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا قَضَى اللَّهُ لِعَبْدٍ أَنْ يَمُوتَ بِأَرْضٍ جَعَلَ لَهُ إِلَيْهَا حَاجَةً».
Imepokelewa kutoka kwa Matwar Bin Ukaamis -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile."
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu akimpangia mtu kuwa afie katika ardhi fulani na hali yakuwa yeye hayupo katika ardhi hiyo; Basi humfanya ahitajie kitu katika ardhi ile hivyo ataenda katika ardhi ile, basi huchukuliwa roho yake akiwa huko.
Mafunzo
- Hadithi inathibitisha maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na nafsi haijui itafia katika ardhi gani."
Marejeo
سنن الترمذي (4/ 23) (2146)، تحفة الأحوذي (6/ 299).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِعَمِّهِ: «قُلْ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، أَشْهَدُ لَكَ بِهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ»، قَالَ: لَوْلَا أَنْ تُعَيِّرَنِي قُرَيْشٌ، يَقُولُونَ: إِنَّمَا حَمَلَهُ عَلَى ذَلِكَ الْجَزَعُ لَأَقْرَرْتُ بِهَا عَيْنَكَ. فَأَنْزَلَ اللهُ: {إِنَّكَ لا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَكِنَّ اللهَ يَهْدِي مَنْ يَشَاءُ } [القصص: 56].
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimwambia baba yake mdogo: "Sema: Laa ilaaha illa llahu, nitakutolea ushuhuda wa kusilimu kwa maneno hayo siku ya Kiyama" Akasema: Ningetamka kama si kuogopea matusi ya Makuraishi wanasema kulichompelekea kusema maneno hayo ni kuogopa kifo, kama si hivyo ningeingiza furaha moyoni mwako, basi Mwenyezi Mungu akateremsha: "Hakika wewe huwezi kumuongoza umtakaye lakini Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye" (suratul Qaswas: 56)
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimtaka Abuu Twalib ambaye ni baba yake mdogo akiwa katika kilevi cha mauti, atamke neno Laa ilaaha illa llahu, ili amuombee utetezi kwa neno hilo siku ya Kiyama, na amtolee ushuhuda wa kusilimu kwake, akakataa kutamka shahada kwa kuogopea kuwa Makuraishi watamtukana na watamsema kuwa: Amesilimu kwa sababu ya kuogopa mauti na unyonge! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kama si huko kuogopa ningeingiza furaha katika moyo wako kwa kutamka kwako shahada na mauti yangekufika kwa namna ambayo ungeiridhia! basi akateremsha Mwenyei Mungu Aya ambayo inajulisha kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hamiliki uongofu wa kuukubali uislamu, bali Mwenyezi Mungu aliyetukuka peke yake humuwezesha amtakaye. Na kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake anawaongoza viumbe kwa ufahamu na kuwawekea wazi na kuwaongoza pamoja na kuwaita kwenye njia iliyonyooka.
Mafunzo
- Haki huwa haiachwi kwa sababu ya maneno ya watu.
- Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anamiliki uongofu wa ufahamishaji na uelekezaji na siyo uongofu wa kukubaliwa.
- Ni katika sheria kumtembelea Kafiri akiwa mgonjwa kwa ajili ya kumlingania katika uislamu.
- Pupa ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika kulingania kuelekea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hali yoyote.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 55) (25)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (1/ 539)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص 742).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ الصَّادِقُ المَصْدُوقُ: «إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ المَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَوْ سَعِيدٍ؛ فَوَالَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا، وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Abdirahman Abdullahi Bin Masoud radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alituhadithia Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye ndiye mkweli mwenye kusadikika: "Hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake ndani ya tumbo la mama yake siku arobaini, kisha linakuwa pande la damu kwa mfano wake, kisha linakuwa pande la nyama mfano wake (siku arobaini), kisha linatumiwa Malaika analipulizia roho, na anaamrishwa kuandika maneno manne: Kuandika riziki yake, na umri wake, na matendo yake, na kuwa ni muovu au mwema; namuapa yule ambaye hakuna Mola isipokuwa yeye hakika mmoja wenu atafanya amali za watu wa Peponi mpaka ikawa baina yake na Peponi ni dhiraa moja (futi) kikamtangulia kitabu akafanya amali za watu wa motoni akauingia, na hakika mmoja wenu atafanya amali za watu wa motoni mpaka ikawa baina yake na Moto isipokuwa dhiraa, kitabu kikamtangulia akafanya amali za watu wa Peponi na akaingia".
Imepokelewa na Bukhari na MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amesema Bin Masoud: Ametuhadithia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake naye ni mkweli kwenye maneno yake, na mwenye kukubaliwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemkubali, Amesema: Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake, na jambo hilo ni kuwa mtu akimuingilia mke wake basi yale manii yake yaliyosambaa hukusanywa kwenye tumbo la mwanamke kwa muda wa siku arobaini yakiwa ni tone la manii, Kisha hubadilika na kuwa pande la damu nzito iliyoganda, haya hufanyika katika arobaini ya pili, Kisha hubadilika kuwa pande la nyama, nacho ni kipande cha nyama chenye ukubwa wa kuweza kutafunwa, na mabadiliko haya ni katika arobaini ya tatu, Kisha Mwenyezi Mungu hulitumia pande hilo la nyama Malaika, kisha hulipulizia ndani yake roho baada ya kuisha siku arobaini za tatu, Na huamrishwa Malaika aandike maneno manne, nayo ni: Riziki yake, nacho ni kiwango ambacho atakipata miongoni mwake ni neema katika umri wake, Na pia huandikwa wakati wake, nao ni muda wa kubakia kwake Duniani, Na matendo yake, yatakuwa ni yapi? Na je atakuwa muovu au mwema. Kisha akaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yawezekana mtu akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa peponi, na yakawa matendo yake ni mazuri, yaani kwenye muonekano wa watu, na akabakia hivyo mpaka inakuwa kati yake na Pepo ni kiasi cha mkono, yaani kiasi kilichobaki kati yake mpaka kuifikia pepo ni kidogo sana kama vile ambavyo mtu amebakiza nafasi kati yake na ardhi kiasi cha mkono, mara Kitabu kinamtangulia na kile alichopangiwa, na wakati huo anafanya matendo ya watu wa motoni na akaandikiwa kuwa huo ndio mwisho wake na akaingia motoni; Kwa sababu sharti la kukubaliwa matendo yake ni kudumu katika matendo hayo na wala asibadilishe, na watu wengine wapo wenye kufanya matendo ya watu wa motoni mpaka mtu anakaribia kuingia motoni, mpaka inakuwa kati yake na kuingia motoni ni kiasi cha urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu na alichopangiwa hivyo akafanya matendo ya watu wa peponi na akaingia peponi.
Mafunzo
- Kumebainishwa hatua za uumbwaji wa mwanadamu.
- Kuamini hukumu na kadari.
- Mwisho wa mambo yote huwa kwa namna ambavyo imekwishapangwa na kukadiriwa.
- Tahadhari ya kutodanganyika na muonekano wa matendo; Bali matendo huangaliwa mwisho wake.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 135) (7454)، (4/ 111) (3208).
صحيح مسلم (4/ 2036) (2643).
عمدة القاري شرح صحيح البخاري (15/ 130).
شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 84).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي العَبَّاسِ، عَبْدِ الله بْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: كُنْت خَلْفَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمًا، فَقَالَ: «يَا غُلَامِ! إنِّي أُعَلِّمُك كَلِمَاتٍ: احْفَظِ اللَّهَ يَحْفَظْكَ، احْفَظِ الله تَجِدْهُ تُجَاهَكَ، إذَا سَأَلْتَ فَاسْأَلِ اللهَ، وَإِذَا اسْتَعَنْتَ فَاسْتَعِنْ بِاَللهِ، وَاعْلَمْ أَنَّ الأُمَّةَ لَوْ اجْتَمَعَتْ عَلَى أَنْ يَنْفَعُوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَنْفَعُوكَ إلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ لَكَ، وَإِنِ اجْتَمَعُوا عَلَى أَنْ يَضُرُّوكَ بِشَيْءٍ لَمْ يَضُرُّوكَ إلَّا بِشَيْءٍ قَدْ كَتَبَهُ اللَّهُ عَلَيْكَ؛ رُفِعَتِ الأَقْلَامُ، وَجَفَّتِ الصُّحُفُ».
وَفِي رِوَايَةِ غَيْرِ التِّرْمِذِيِّ: «احْفَظِ اللهَ تَجِدْهُ أَمَامَكَ، تَعَرَّفْ إلَى اللهِ فِي الرَّخَاءِ يَعْرِفْكَ فِي الشِّدَّةِ، وَاعْلَمْ أَنَّ مَا أَخْطَأَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبَكَ، وَمَا أَصَابَك لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَاعْلَمْ أَنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنْ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرًا».
Kutoka kwa Abul-Abbas, Abdallah bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema: Siku moja nilikuwa nyuma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ewe kijana, hakika mimi ninakufundisha maneno: Muhifadhi Mwenyezi Mungu naye atakuhifadhi, muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta uendako, utakapo omba basi muombe Mwenyezi Mungu, na ukitaka msaada muombe msaada Mwenyezi Mungu, na tambua: kuwa laiti watu wote wangelikusanyika ili wakunufaishe wewe kwa kitu chochote, hawatoweza kukunufaisha isipokuwa kwa kitu ambacho tayari kakiandika Mwenyezi Mungu kwako, na ikiwa watakusanyika kwa ajili ya kukudhuru wewe kwa kitu chochote, hawatoweza kukudhuru kwa kitu chochote isipokuwa kile ambacho kakuandikia Mwenyezi Mungu kikupate, kalamu zimenyanyuliwa na kurasa zimekauka" Na katika riwaya isiyokuwa ya Tirmidhi: "Muhifadhi Mwenyezi Mungu utamkuta mbele yako, Jipendekeze kwa Mwenyezi Mungu wakati wa raha atakujua wakati wa shida, na tambua kuwa yaliyo kukosa hayakua ni yenye kukupata, na yaliyo kupata hayakuwa ni yenye kukukosa, na tambua kuwa msada huambatana na subira, na kuwa faraja huwa pamoja na matatizo, na kuwa uzito huwa pamoja na wepesi".
Imepokelewa naTirmidhiy na wengineoDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza bin Abbas -radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa yeye alipokuwa kijana mdogo alikuwa kapanda pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akasema kumwambia -Amani iwe juu yake-: Hakika mimi ninakufundisha vitu na mambo ambayo Mwenyezi Mungu atakunufaisha kwayo: Muhifadhi Mwenyezi Mungu kwa kuhifadhi maamrisho yake na kuepuka makatazo yake, kiasi kwamba akukute katika utiifu na yale yenye kukuweka karibu naye, na asikukute katika maasi na madhambi, ikiwa utafanya hivyo basi malipo yako yatakuwa ni Mwenyezi Mungu kukuhifadhi kutokana na kero za Dunia na Akhera, na atakunusuru katika mambo yako magumu mahala popote utakapoelekea. Na ukitaka kuomba jambo, basi usimuombe ila Mwenyezi Mungu kwani Yeye pekee ndiye mwenye kuwajibu waombaji. Na ukitaka msaada basi usiutake ila kwa Mwenyezi Mungu. Na uwe na yakini kuwa hutopata manufaa yoyote hata kama viumbe wote wa Ardhini watakusanyika ili kutaka kukunufaisha, isipokuwa kwa kile alichokiandika Mwenyezi Mungu kwako, na wala hutopata madhara hata kama viumbe wote wa Ardhini watakusanyika ili kutaka kukudhuru, isipokuwa kwa lile alilolikadiria Mwenyezi Mungu juu yako. Na kuwa jambo hili kashaliandika Mwenyezi Mungu Mtukufu na akalikadiria kulingana na namna hekima na elimu yake zilivyopelekea, na hakuna kubadilishwa yale aliyoyaandika Mwenyezi Mungu. Na kwamba atakayemuhifadhi Mwenyezi Mungu kwa kuhifadhi amri zake na kuyaepuka makatazo yake; basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atakuwa mbele ya mja kwa kuyajua matatizo yatakayomfika na atamnusuru na kumpa msaada. Na kwamba mwanadamu atakapomtii Mwenyezi Mungu wakati wa raha basi Mwenyezi Mungu atamletea faraja na njia ya kutokea wakati wa shida, hivyo na aridhie kila mja na kile alichokikadiria Mwenyezi Mungu cha kheri na shari. Na kukiwa na matatizo na mitihani basi mja ashikamane na subira kwani subira ni ufunguo wa faraja, na kwamba mitihani ikizidi kuwa mingi ndio faraja huja kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba uzito unapotokea Mwenyezi Mungu huufuatisha na wepesi.
Mafunzo
- Umuhimu wa kuwafundisha vijana na watoto wadogo mambo ya dini kuanzia Tauhidi na adabu na mengineyo.
- Malipo huenda sawa na matendo.
- Amri ya kumtegemea Mwenyezi Mungu, na kutawakali kwake bila kumtegemea asiyekuwa yeye, na yeye ndiye msaidizi bora.
- Kuamini maamuzi na mipango ya Mwenyezi Mungu na kuridhika nayo, nakuwa Mwenyezi Mungu amekwisha kadiria kila kitu.
- Atakayetelekeza amri ya Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu naye humtelekeza na humnyima ulinzi.
- Habari njema kubwa kwa mwanadamu kuwa pale unapompata uzito basi asubiri wepesi.
- Kuliwazwa mja pale inapotokea mitihani, na kuyakosa yale ayapendayo, kwa mujibu wa kauli yake: "Na tambua kuwa yaliyokufika hayakuwa ni yenye kukukosa, na yaliyokukosa hayakuwa ni yenye kukupata" Sentensi ya kwanza ni kuliwazwa wakati wa kufikwa na yenye kuchukiza, na ya pili ni katika kuyakosa yale yenye kupendeka.
Marejeo
سنن الترمذي (4/ 284) (2516).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية (ص42).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص200).
فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، للعباد (ص69).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com